2013-11-06 15:11:25

Baraza la Makanisa Ulimwengu limechagua wajumbe wa 150 wa Kamati kuu


Wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Jumatano tarehe 6 Novemba 2013 wamechagua Kamati kuu ya Baraza inayojumuisha wanachama 150, watakaokuwa na dhamana la kutoa maamuzi kati ya mikutano mikuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni.

Wawakilishi hao asilimi 39% ni wanawake, asilimia 61% ni wanaume; vijana wanaunda asilimia 13%, wawakilishi kutoka katika makundi asilimia ni asilimia 5% na watu wenye ulemavu wanaunda asilimia 2%. Kati yao Makleri ni asilimia 68% na Waamini walei ni asilimia 32. Majina haya yamechaguliwa kutoka katika majina yaliyokuwa yamependekezwa na wajumbe 345 wa Makanisa wanachama.







All the contents on this site are copyrighted ©.