Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim,
Jumatatu walianza ziara ya pamoja kutembelea Mkoa wa Sahel Afrika Kaskazini. Kufuatia
ziara hii ya kihistoria ya viongozi hao wawili , Benk ya Dunia na Umoja wa Ulaya ,
Jumatatu uliahidi kutoa kiasi cha $bilioni 8.2 kwa ajili ya kukuza uchumi na kupambana
na ufukara katika eneo la Sahel. EU ikiahidi msaada wa $6.7 biliioni katika kipindi
cha miaka saba ijayo , na benk ya dunia itatoa msaada wa dola Billioni $1.5 katika
kipindi cha miaka miwili. Katika ziara hiìi , viongozi hawa kwa pamoja wanazuru
Mali, Niger, Burkina Faso na Chad. Na mara walipowasili Bamako Katibu Mkuu Ban Ki
mon, alizungumza na waandishi wa habari kuelezea kwa nini yeye na viongozi wengine
wa dunia, wanakwenda katika ukanda wa Sahel, pamoja, ambako watahudhuria Mkutano
wa Mkoa wa Mawaziri unaofanyika Bamako Mali. Viongozi wengine wa ngazi ya juu
wanaoshiriki katika ziara hii ni pamoja na Andris Piebalgs , Kamisheni katika Tume
ya Umoja wa Ulaya kwa ajili ya Maendeleo , pia Nkosazana Dlamini Zuma , MwenyekIti
wa Tume Tendaji ya Umoja wa Afrika, na Rais Donald Kaberuka , wa Benk ya Maendeleo
ya Afrika. Ban na Yong Kim wamewasili Mali wakionyesha kujali changamoto za kutisha
zinazo jitokeza katika eneo hili, licha ya maafa ya kihali pia kuna mauaji ya makusudi
kama ilivyofanyika kwa waandishi wawili wa Kifaransa waliouawa hivi karibuni. Wameonyesha
kishawishi chao kwamba, mduara huu wa kipeo katika eneo la Sahel, unaweza kuvunjwa
na mkoa huo kusonga mbele kutokana hali za wasiwasi na kuwa na uhakika wa maisha na
maendeleo. Mkoa wa Sahel ni eneo kame Kusini mwa jangawa la Sahara linalotambaa
Kaskazini mwa Afrika tangu Mauritania hadi Eritrea, ambako, katika kipindi cha miaka
kumi iliyopita, limekuwa na ukame wa kukithiri kwa zaidi ya mara tatu, ikitishia
maisha ya watu zaidi ya millioni 11 wa eneo hilo, hasa kwa watoto walio chini ya
umri wa miaka mitano wapatao milioni tano.