Sikiliza "The Original Comedy" ya Zakayo mtoza ushuru aliyeparamia Mkuyu ili kumwona
Yesu!
Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki Watanzania wanaosoma mjini Roma pamoja na watanzania
katika ujumla wao, Jumapili iliyopita, tarehe 3 Novemba 2013 waliadhimisha Ibada ya
Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakaribisha wanafunzi wapya, kumkumbuka na kumwombea
Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na kuungana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
katika Maandalizi ya Kufunga Mwaka wa Imani, huko Bagamoyo, Jumapili tarehe 10 Novemba
2013.
Ibada hii
ya Misa Takatifu iliongozwa na Mheshimiwa Padre Alcuin Nyirenda. OSB na kuhudhuriwa
na umati mkubwa wa Mapadre, Watawa, Waseminari na Waamini walei. Katika mahubiri yake,
Padre Nyirenda aligusia kwa namna ya pekee vituko vya maisha ya Zakayo; tajiri na
mkuu wa watoza ushuru akikwea juu ya Mkuyu kwani alitamani kumwona Yesu.
Licha
ya mali na utajiri; cheo na dhamana aliyokuwa nayo ndani ya Jamii, bado alikosa amani,
utulivu wa ndani na furaha hadi pale alipokutana na Yesu, akamkirimia: amani, furaha
na wokovu! Akamwonjesha huruma na upendo wa Mungu kwa kumwita kwa jina!