Wajumbe wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, WCC, Jumatatu tarehe 4 Novemba 2013 wamefanya
uchaguzi wa Marais kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaounda kanda za Uongozi.
Mkutano huu umefanyika katika kikao cha faragha, katika mkutano mkuu wa kumi wa Baraza
la Makanisa Ulimwenguni unaoendelea mjini Busan, Korea ya Kusini.
Marais waliochaguliwa
wanadhamana ya kuhamasisha majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa pamoja na
kutafsiri kwa vitendo maamuzi ya mkutano mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni kadiri
ya maeneo wanayowakilisha. Mkutano huu pia unatarajiwa kuwachagua wajumbe wa Kamati
kuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni.
Marais waliochaguliwa ni pamoja na: 1.
Afrika: Rev. Dr. Mary Anne Plaatjies Van Huffel, kutoka Afrika ya Kusini. 2. Asia:
Prof. Dr. Sang Chang, kutoka Korea. 3. Ulaya: Askofu mkuu Anders Wejryd kutoka
Sweden. 4. Amerika ya Kusini na Caribbean: Rev. Gloria N. U. Alvardo, kutoka Colombia. 5.
Amerika ya Kaskazini: Askofu Mark Macdonald kutoka Canada. 6. Visiwa vya Pacific:
Rev. Dr. Mele'ana Puloka kutoka Visiwa vya Tonga. 7. Waorthodox wa Mashariki: Patriaki
John X kutoka Antiokia. 8. Waorthodox wa Magharibi: Patriaki Karekini II kutoka
Armenia.