2013-11-02 11:21:18

Makardinali 7 na Maaskofu 136 wamefariki dunia katika kipindi cha Mwaka 2012-2013


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 4 Novemba anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwaka 2013. Ibada hii itafanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican majira ya asubuhi. Katika kipindi hiki, Makardinali 7 na Maaskofu 136 wamefariki dunia, kati yao 17 ni kutoka Barani Afrika.

Kutoka Afrika, Kanisa limempoteza Kardinali Medardo Joseph Mazombwe, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Lusaka, Zambia aliyefariki dunia hapo tarehe 29 Agosti 2013.

Kanisa Barani Afrika linaomboleza vifo vya Maaskofu wafuatao:
1. Askofu mkuu mstaafu Henry Ernest Karlen, Jimbo kuu la Bulawayo, Zimbabwe.
2. Askofu Aloysius Balina, Jimbo Katoliki Shinyanga, Tanzania.
3. Askofu mstaafu Patrick Francis Sheehan wa Jimbo Katoliki Kano, Nigeria.
4. Askofu mkuu Ambrose Madtha, Balozi wa Vatican Pwani ya Pembe.
5. Askofu mstaafu Augugustin Sagna wa Jimbo Katoliki Ziguinchor, Senegal.
6. Askofu mstaafu John Martin Darko wa Jimbo Katoliki Sekondi-Takoradi, Ghana.
7. Askofu Joseph O. Egerega, wa Jimbo Katoliki Bomadi, Nigeria.
8. Askofu mstaafu Ignace Sambar Talkena wa Jimbo Katoliki la Kara, Togo.
9. Askofu mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki Moshi, Tanzania.
10. Askofu mstaafu Gerald Sithunywa Ndlovu wa Jimbo Katoliki la Umzimkulu, Afrika ya Kusini.
11. Askofu mstaafu Akio Johnson Mutek wa Jimbo Katoliki Torit, Sudan ya Kusini.
12. Askofu mstaafu Felix Ramananarivo wa Jimbo Katoliki Antsirabè, Madagascar.
13. Askofu mkuu mstaafu Dominic Kodwo Andoh, Jimbo Katoliki la Accra, Ghana.
14. Askofu mkuu mstaafu Michael Kpakala Francis, Jimbo kuu la Monrovia, Liberia.
15. Askofu mstaafu Luis Gonzaga Ferreira da Silva, Jimbo Katoliki Lichinga, Msumbiji.
16. Askofu mstaafu Bernardo Filipè Governo wa Jimbo Katoliki Quelimane, Msumbiji.
17. Askofu mstaafu Raymond Mwanyika wa Jimbo Katoliki Njombe, Tanzania.

Hii ndiyo orodha ya Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia hadi kufikia tarehe 2 Novemba 2013 wakati tukiwa tunaandika taarifa hii.

Raha ya milele uwape Ee Bwana na Mwanga wa Milele uwaangazie, wapumzike kwa Amani, Amina.







All the contents on this site are copyrighted ©.