2013-11-01 15:53:12

Siku Kuu ya Watakatifu wote hutukumbusha uwepo wetu duniani si kwa ajili ya kifo bali ni Paradiso- Papa


Baba Mtakaifu Francisko, Ijumaa hii wakati wa sala ya Malaika wa Bwana aliwasalimia mahujaji na wageni na kundi la watu walioshiriki katika mbio za Watakatifu, kundi lililokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Hotuba yake aliangalisha katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Watakatifu wote akisema, Siku Kuu hii hutukumbusha sote kwamba, lengo la uwepo wetu si kifo bali ni kwa ajili wa Paradiso, kama alivyoandika Mtume Yohana: sisi ni watoto wa Mungu, lakini bado haija onekana wazi jinsi tutakavyokuwa ila tunajua wazi kwamba , wakati Kristo atakakuja, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo " (1Yoh 3:02 ).
Watakatifu na marafiki wa Mungu, wanatuhakikishia, ahadi hii ya Mungu ambayo haitahayarishi. Katika maisha yao ya kidunia kweli waliishi katika ushirika mkubwa na Mungu. Na kupitia sura za ndugu hawa wadogo na walionyanyasika , waliweza kuiona sura ya Mungu , na sasa wanazunguzma nae uso kwa uso katika uzuri wa utukufu wake. .

Papa alieleza na kuweka bayana kwamba Watakatifu tunaowataja hawakuwa viumbe wa kipekee, wala kwamba walizaliwa wakiwa wakamilifu. Walikuwa watu kama sisi sote, na kila mmoja wetu, ni watu ambao kabla ya kufikia utukufu wa mbinguni wamekuwa wakiishi maisha ya kawaida, katika hali za furaha na huzuni , mapambano na matumaini.
Lakini kuna jambo lililowabadilisha katika maisha yao , nalo ni kuujua upendo wa Mungu, na kuufuata kwa moyo wao wote, kwa ukweli na bila unafiki, ni watu walio yatumia maisha yao katika utumishi wa wengine, wakivumilia shida na sulubu za mateso, bila chuki katika kukabiliana na uovu, wakwia wamejawa na furaha ya uzuri wa kueneza imani na amani.

Papa amewataja Watakatifu wote wake kwa waume, kuwa ni urithi mkubwa katika historia ya wabatizwa wote. Na amesisitiza kwamba si upendeleo kwa wachache lakini ni wito kwa kila mmoja. Papa amesema, sote tuna uwezo wa kuwa Watakatifu katika Ubatizo na ni wito kwa kila mtu.
Huu ni mwaliko kwa watu wote, ni wito wa kutembea katika njia ya utakatifu, ambayo inaongozwa na Jina Takatifu Yesu Kristu, ni kutembea ana kwa ana Kristu. Yeye anatufundisha kuwa watu wa Mungu, anatuonyesha njia ya Heri (taz. Mt 5:1-12)
Na wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Papa alisalimia makundi mbalimbali ya walioshiriki katika Ibada hii na wote walioshiriki asubuhi hii katika mbio ya Watakatifu, iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha wa Don Bosco katika ulimwengu. Papa akirejea tukio alimrejea Mtakatifu Paulo aliyesema kwamba, maisha yote ya Kikristo ni mbio za kushinda tuzo ya utakatifu. Papa aliwashukuru washindani wote .
Nyakati za jioni , Papa alielekea katika eneo la Verano , ambako emeongoza Ibada ya Misa katika lango kuu la Makaburi ya Kirumi ya Verano ya jijini Roma. Na baada ya Ibada hiyo , aliongoza sala kwa ajii ya kuwaombea Marehemu wote na kutoa baraka wka makaburi hayo.
Papa ameongoza liturujia ya maadhmisho haya kisaidiana na Vika Mkuu wa Jimbo la Roma, Kardinali Agostino Vallini, na pia Askofu Mkuu Filippo Iannone, Makamu Vika wa Jimbo la Roma, Maaskofu wasaidizi na Paroko wa Basilika la Mtakatifu Lawrence Nje ya kuta, Padre Armando Ambrosi.
Makaburi haya kwa mara yamwisho yalitembelewa na Papa Yohane Paulo II, Novemba 1, 1993, miaka ishirini iliyopita kwa ajiliya maadhimisho ya Sik Kuu ya Watakatifu wote.







All the contents on this site are copyrighted ©.