2013-11-01 15:59:20

Askofu Mkuu Boniface Lele astaafu


Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa hii, mosi Novemba 2013, amekubali ombi la kustaafu la Askofu Mkuu Boniface Lele, kuwa mtawala wa kichungaji kwa Jimbo Kuu la Mombasa, kwa mujibu wa sheria ya Kanisa namba 401/2.

Kwenye nafasi yake Papa amemteua Askofu Emmanuel Barbera , wa Jimbo la Malindi, kuwa Msimamizi wa Kitume kwa jimbo Kuu la Mombasa.

Askofu Mkuu Boniface Lele, alizaliwa 1947, Kitui Kenya. Alipadrishwa tarehe 8 Decemba 1974. Aliteuliwa kuwa Askofu Novemba 15, 1995, na kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mombasa, tarehe 25 June 2005.








All the contents on this site are copyrighted ©.