Salaam za Papa Francisko kwa Mkutano Mkuu wa WCC : Aomba mshikamano wa dhati.
Papa Francisko ametoa wito kwa Wakristo wote , kuimarisha maombi, sala na ushirikiano,
kwa ajili huduma ya Injili. Wito huo umo katika barua yake kwa washiriki wa Mkutano
wa Kumi Mkuu wa Baraza la Makanisa Duniani, unaofanyika Busan, Korea ya Kusini. Rais
wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo , Kardinali Kurt Koch, Jumatano
alisoma barua hiyo ya Papa , ambamo anawahimiza Wakristo wote, kuona kwamba, wameitwa
kuwafikia wale ambao wanajikuta wamewekwa pembezoni na jamii hasa iliyoendelea.
Na kwamba, Wakristu kama familia ya Mungu , wanapaswa kuonyesha mshikamano na wale
wanaoishi mazingira magumu zaidi wanawake kwa wanaume, watu maskini, walemavu, hata
wale ambao bado kuzaliwa, wagonjwa, wahamiaji na wakimbizi , wazee na vijana ambao
hawana ajira.
Papa Francisko ameitumia nafasi hii pia kutoa shukurani za dhati
kwashiriki wa mkutano huu, wa Busan, na kwa namna ya pekee kwa Katibu Mkuu , Dr Olav
Fykse Tveit , na wawakilishi ya jamii ya Kikristo. Papa amewahakikishia sala zake
na ukaribu wake wakati huu wa mkutano na pia katika uwajibikaji wa kanisa Katoliki
kwenye mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu na na Baraza la Makanisa la Dunia.
Papa anasema, mandhari ya Mkutano huu wa Busan, ni "Mungu wa Maisha, tuongoze
katika Haki na Amani" tayari ni ombi kwa Utatu Mtakatifu wa Mungu, ambaye huvileta
viumbe vyote katika utimilifu, kwa njia ya nguvu ya ukombozi ya Msalaba wa Yesu Kristo
na kwa namna nyingi za zawadi za Roho Mtakatifu. Kwa hakika , kila mahali ambapo zawadi
ya Maisha huheshimiwa, haki na amani kutawala , mahali hapo upo Ufalme wa Mungu na
uwezo wake uko tayari kufanya kazi. Kwa sababu hii, Papa ameonyesha tumaini lake
kwamba, uwepo wa mkutano huu wa Busan, utaweza kusaidia kuimrisha dhamiri ya wafuasi
wa Kristu kattika maombi na ushirikiano katika huduma, na mwingiliano wa utendaji
katika familia ya binadamu, kwa ajili ya ufanikisha mazuri kwa watu wote. Katika
dunia hii ya utandawazi Papa ameendelea,Wakristu wanatakiwa kushuhuduia kwa pamoja
, heshima ya utu wa Mtu aliyopewa na Mwenyezi Mungu, na kukuza utamaduni na sheria
za kijamii zinazomruhusu kila mwanadamu na kukuza ufanisi katika mazingira ya kitamaduni,
kijamii na kisheria, ili kuwezesha watu binafsi na jamii kwa ujumla kukua katika uhuru,
na ambao ni msaada msingi kwa familia, kujenga jamii katika mshikamano thabiti katika
majiundo na utoaji wa elimu ni muhimu kwa vijana , na kwa ajili ya kuthamini utendaji
usioweza kukwepa wa uhuru wa kidini. Na kwa uaminifu wa injili, na katika kukabiliana
na mahitaji ya dharura ya wakati huu wetu, tunatakiwa kuwafikia wale ambao wameachwa
pembezoni na jamii na kuonyesha mshikamano nao, hasa wale wanaoishi katika mazingira
magumu, wake kwa waume, maskini, walemavu, na wale ambao hawajazaliwa, wagonjwa,
wahamiaji na wakimbizi , wazee na vijana ambao hawana ajira.
Kwa ufahamu kwamba,
wa moyo wa kiekumeni unabaki kuwa uongofu wa kweli takatifu ( taz. Unitatis Redintegratio
, 8) , Papa anasali kwa ajili ya Mkutano Mkuu huo, ili uweze kuchangia katika kutoa
msukumo mpya wa uhai na matazamio katika sehemu ya uwajibikaji wote wa mchakato mtakatifu
unaotafuta Umoja kamili wa Wakristu , katika uaminifu wa mapenzi ya Bwana kwa Kanisa
lake (taz. Yn 17:21 ) na katika uwazi wa unaokuzwa Roho Mtakatifu. Kwao wote
washiriki wa Mkutano huu wa Busan , Papa amewapa Baraka zake za Kitume na kuwaombea
Baraka tele za Mwenyezi Mungu, chanzo cha maisha yote na kila zawadi ya kiroho.