2013-10-31 11:14:15

Rais Putin kukutana na Papa Francisko mwishoni mwa Mwezi Novemba?


Serikali ya Russia inaangalia uwezekano wa Rais Vladimir Putin kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francesko, mwishoni mwa Mwezi Novemba, wakati Rais wa Russia atakapokuwa nchini Italia kwa mwaliko wa Serikali ya Italia. Kama mipango hii itakwenda kadiri inavyosikika kwa sasa, hii itakuwa ni mara ya kwanza Rais wa Russia kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu.

Shirika la Habari la Zenith linabainisha kwamba, kwa sasa Ikulu ya Russia inaendelea kufanya mazungumzo na Ikulu ya Italia kuhusu ratiba na uwezekano wa viongozi hawa wawili kukutana. Italia na Russia itakuwa na mkutano wa pamoja mjini Trieste mwishoni mwa Mwezi Novemba na baadaye ujumbe wa Russia utatembelea pia mjini Roma.







All the contents on this site are copyrighted ©.