Vatican yapanda hadhi katika kipimo cha uwazi kwenye masuala ya fedha
Wakala wa Kujitegemea katika upimaji wa viwango vya uadilifu kwenye masuala yanayohusiana
na fedha na Benki “The Standard Ethics Rating (SER)”, Jumatatu walitangaza kupandisha
hadhi Nchi ya Jiji la Vatican katika kipimo cha ubora wa usimamizi na uwazi kwenye
masuala ya fedha .
Shirika hili la SER, ni chombo kinacho pima hali katika
masuala ya uendelevu , wajibu wa kijamii , utawala bora na mazingira yanayohusiana
na masuala ya fedha haswa uhamishaji wa fedha kutoka akaunti moja hadi nyingine. Taarifa
inasema, Vatican imeonyesha jitihada chanya na endelevu, katika kipimo cha uboreshaji
wa maadili katika mifumo yake ya fedha na jamii, kama matokeo ya kazi na takwimu
za kisayansi zilizo fanywa hapa na pale katika dunia ya uchumi kwenye uhusiano wa
kanuni za maadili zinazozingatiwa na mashirika makubwa ya kimataifa.
Na kwamba,
SER, tangu ilipopewa mtazamo chanya Julai iliyopita , kwa kazi zake za kusimamia
masuala ya fedha Vatican, Jiji la Vatican limefanikisha matwaka ya kimataifa yanayo
dai uwazi zaidi katika akaunti za Vatican na taasisi zake za kifedha.
Na
pia inafafanua kwamba , Vatican ilitakiwa kuchukua hatua muhimu dhidi ya utakatifushaji
fedha wa haramu, au fedha kutumika katika matendo haramu au ufadhili wa ugaidi
kwa fedha zinazotoka au kuingia katika Benk yaVatican au taasisi zake za fedha. Vatican
imweze kuzingatia taratibu na vigezo vilivyo wekwa na Jopo la Utendaji la Kujitegemea”Financial
Action Task Force” (Groupe d' Financière FATF - GAFI ) kama ilivyo pitishwa katika
mapendekezo kutoka Idara Moneyval ya Baraza la Ulaya .
Aidha, ripoti inaeleza
kwamba hatua muhimu zillizo chukuliwa, zimefanikishwa na Tume ya Kipapa kwa ajili
ya utawala wa nchi ya Jiji la Vatican, kwa sheria yake namba XVIII ya Oktoba 8, 2013
. Sheria hii inafanikisha uwepo wa chombo kinachosimamia uwazi, usimamizi na utoaji
wa taarifa za fedha . Sheria mpya ni matunda ya Katiba ya miaka michache iliyopita
ya Mamlaka ya Habari wa Fedha ( AIF ).
Na pia kwamba, Mambo zaidi ya uwazi
na ripoti na matamko , yamefanikisha uchapishaji wa Ripoti ya Mwaka ya Shughuli
ya Fedha, na Mwaka wa kwanza wa AIF 2012, pia uchapishaji wa ripoti ya kila mwaka
kwenye tovuti ya Benki ya Vatican ( Istituto kwa le Opere Religiose IOR ) iliyotoka
tarehe 1 Oktoba 2013.