2013-10-28 15:30:14

Papa Francisko aliweka taifa ya Equatoria Quinea chini ya ulinzi wa Maria.


Jumapili , Papa Francisko aliikamilisha Ibada ya Misa aliyo iongoza katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kwa sala ya Malaika wa Bwana. Alisema kabla ya kufunga Ibada hii , nina hamu kubwa ya kutoa salaam zangu kwa mahujaji wote, na hasa kwa familia zilizokusanyika kwa wingi katika Ibada hii.

Na pia kwa moyo wa upendo mkuu, ushariki na umoja alitoa salaam zake za Maaskofu wote , na kwa waamini wa Guinea Equatoria, taifa ambamo siku ya Ijumaa, 25 Oktoba 2013, lilibadilishana itifaki ya ushirikiano na serikali ya Vatican. Ujumbe ulioongozwa na Rais wa Guinea Equatoria, Teodre Obiong Guema Mabasogo. Papa alitolea sala zake kwa ajili ya taifa hili na kuliweka chini ya ulinzi wa Mama Maria asiyekuwa na doa anayependwa na watu wa Gunea Equatoria, pia akiwataka wadumu katika njia ya maridhiano na haki.

Papa aliendelea kutolea sala zake, akiomba pia ulinzi wa Mama Maria kwa ajili ya familia zote duniani , na kwa namna ya pekee ,wale wanaoishi katika mazingira magumu. Kwa ajili yao, Papa aliwaomba watu wote walioshiriki katika Ibada hii, kusali pamoja nae kwa mara tatu : Maria , Malkia wa Familia utuombee.

Alihimitimisha na Asante kwao wote, walio shiriki katiak ibada hii na pia katika Mkesha wa Jumamosi na kuwapa baraka zake za kitume akisema, Mungu awabariki nyote.










All the contents on this site are copyrighted ©.