2013-10-28 16:17:00

Papa akutana na viongozi na wafanyakazi wa CTV


Baba Mtakatifu Jumatatu 28 Oktoba, akiwa katika ukumbi wa Clementina ndani ya Vatican, aliwataka viongozi na wafanyakazi katika wa kituo cha Runinga cha Vatican, kufanyakazi kwa ushirikiano na mshikamano, kama ule timu ya mpira. Kituo hiki Runinga cha Vatican kilicho zinduliwa rasmi na Mwenye Heri Papa Yohane Paulo II, tarehe 22 Oktoba 1983, kiko katika tafakari za mafanikio na vikwazo, baada ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. .

Katika hotuba yake, pamoja na kutoa shukurani za dhati kwa viongozi na wafanyakazi wa kituo hicho, kazi aliyoitaja kuwa nyeti na muhimu katika kazi za Kichungaji katika uwanja wa Mawasiliano, alisema, kwanza ni lazima na ni muhimu sana kufanya kazi kama timu moja. Kucheza kama timu ya mpira, hasa ufanisi wa huduma ya kichungaji katika mawasiliano. Ufanisi huo unaweza kutoa mwanya au uwezekano wa kutengeneza viungo katika kufanya mageuzi kwa ajili ya uwepo wa ujenzi wa umoja na ushirikiano zaidi katika utoaji wa habari sahihi na ukweli, kwa kufunikwa na nia, lengo na nguvu moja, kama ilivyoelezwa katika Agizo "Inter Mirifica 21". Papa alionyesha kutambua kwamba hili si rahisi, lakini inaweza kwua ni msaada wa kuanza uundaji wa suhirikiano, kama timu, na zaidi ya yote , pia kama dira ya utendaji wenye kushuhudia muungano wao. . .

Pia alikumbusha kwa upande huu wa mawasiliano , wao ndiyo wataalam katika huduma ya Kanisa. Na hivyo kwa unyeti wa kazi yao, unapaswa iwe,kwa ajili ya kutoa mwangwi wa mafundisho ya Kanisa, katika kila kitu, katika sinema , habari, , makala za wahariri, utawala ... Kila kitu kifanyike kwa mtindo na mtazamo kwamba, ni Kanisa, Kanisa Takatifu.

Pia amewaasa kuzingatia kwamba , mwasiliano ya CTV, yasiwe fedheha mbele ya watazamaji, waamini na wale walio mbali na imani , bali mipango yote ya utangazaji, iwe ni uvuvio wa harufu nzuri ya tumaini la Injili.

Mwanzo wa hotuba hii, Papa alitoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu , kwa yale yote aliyo ajalia kazi zake za nyingi za miaka 30 za kituo hiki , ambacho mpaka sasa kinaendelea kupambana na changamoto nyingi za kiteknolojia, kama alivyokwisha watamkia tena katika ujumbe wake , alioutoa kwao hivi karibuni kupitia mkutano wao. Papa amezitaja changamoto hizo kuwa ni halisi wanazotakiwa kukabiliana nazo kwa ushujaa zaidi , ili kuweza kudumisha mtazamo wa kiinjili katika aina hii ya barabara kuu ya kimataifa ya mawasiliano. Papa alipeleka ujumbe kwa CTV , Oktoba 18, 2013m wakati wakianza mkutano wao..

Jumatatu hii, Papa alihitimisha kwa kuwashukuru wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi, wanaosaidia kukiongoza chombo hiki cha CTV, kwa busara na hekima. Pia Papa aliwakumbuka marafiki ambao hushiriki pia katika kazi mbalimbali na kwa nyadhifa mbalimbali katika familia kubwa ya CTV . Alikiri, peke yao hawezi kufanya mengi, lakini kwa pamoja wanaweza kutoa huduma nzuri duniani kote, kueneza ukweli na uzuri wa injili mpaka miisho ya dunia.








All the contents on this site are copyrighted ©.