Yesu anaendelea kuomba kwa ajili yetu, akimwonyesha Baba thamani ya wokovu wetu,
tulioupta kupitia vidonda vyake vya Msalabani. Maneno haya ni msisitizo wa mahubiri
ya Papa Francisko, alioutoa katika Ibada ya Misa, mapema Jumatatu hii. Ibada aliyoiongoza
katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Homilia hiyo iliangalishwa katika
Injili ya siku kwa ajili ya maadhimisho ya Watakatifu Simon na Yuda Mitume .
Kiini
cha homilia ya Papa , kililenga zaidi katika kifungu za Injili ambamo Yesu aliutumia
muda wote wa usiku katika maombi , kabla ya kuchagua mitume wake kumi na wawili.Yesu
anatengenza timu yake, Papa alisisitiza. Na mara baada ya tukio hili, akiwa amezungukwa
na umati mkubwa wa watu, waliofika kumsikiliza na kuponywa Naye, kwake Yeye ambaye
mlitoka nguvu za uponyaji kwa wote. Papa ametafakari Injili hiyo akisema, hapa
tunaona mambo matatu. Yesu katika mahusiano na Baba yake, Yesu na Mitume wake na
Yesu na watu. Yesu aliomba kwa Baba kwa ajili ya Mitume na kwa ajili watu. Na hata
leo hii , bado anaomba kwa ajili ya wale wanaomwomba Mungu na yuko pamoja na wale
wanaomwomba Mungu. Papa aliwahimiza waliokuwa wakimsikiliza kuwa na imani kwamba,Yesu
tunayesali mbele yake ndiye aliyetukomboa kwa sadaka ya maisha yake, na kutuhalalisha
sisi kuitwa wana wa Mungu, kwa mastahili yote. Na kwa sasa ameondoka lakini bado anaomba
kwa ajili yetu. Papa alihoji iwapo Yesu ni i roho? Na kutoa jibu kwamba, la, Yesu
si Roho, bali Yesu ni mtu , mtu aliyemwilishwa na kuwa na mwili kama wetu lakini
katika utukufu wake Mungu. . Yesu ana majeraha kwenye mikono , miguu, ubavu , na wakati
anaomba kwa Baba, anaonyesha thamani ya haki ya kuomba kwa ajili yetu, kama akisema,
" Baba, wote ulionipatia asipotee hata mmoja wao" hivyo tunaimani kwamba waamini hakuna
atakayepotea"
Yesu pia ni kichwa cha maombi yetu, kwa sababu ni yeye aliomba
kwanza, kama ndugu yetu na binadamu kama sisi, na bado anatuombea.
Papa
alitoa wito kwa wote , kumwombea pia akisema, ee Bwana, Wewe ni mwombezi wangu. Alirudia
kusisitiza, Yesu anaomba kwa ajili yangu, anaomba kwa sisi wote na anaomba kwa Baba
ushujaa, akionyesha vidonda vyake kuwa dhamana ya haki yetu kuitwa wana wa Mungu.
Papa amemtaka kila muumini afikiri sana kuhusu hili, na kumshukuru Bwana kwa wema
wake uliotupa stahili hii. Asante kwa ndugu yetu anayejumuika nasi katika kuomba kwa
ajili yetu. Maombezi kwa ajili yetu. Papa anasemqa, basi yatupasa sisi pia kuzungumza
na Yesu, na kumwambia: Bwana, Wewe ni mwombezi wangu , na mwokozi wangu, uliyenipa
mastahili ya haki. Katika maombi yetu , tukabidhi kwake yeye Mwombezi wetu, matatizo
yetu, maisha yetu, mambo mengi yote kwake, ili ayafikishe kwa Baba , aliyemtuma yey
kuja duniani kutukomboa dhdi ya mwovu .