Viongozi wapongeza uhusiano mzuri kati ya Kanisa na Serikali nchini Panama
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi, tarehe 26 Oktoba 2013 amekutana na kuzungumza
na Rais Riccardo Alberto Martinelli Berrocal wa Panama na baadaye wamekutana pia na
Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano
wa kimataifa mjini Vatican.
Viongozi hawa wamezungumzia hali ya maisha nchini
Panama na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuhusu masuala ya kijamii na mipango ya
maendeleo endelevu. Viongozi hawa wawili wamepongeza uhusiano mzuri uliopo kati ya
Kanisa na Serikali kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Panama.
Rais
wa Panama amemzawadia Baba Mtakatifu Francisko Sanamu ya Bikira Maria wa Antiqua ambayo
imepamba tayari kwenye bustani za mji wa Vatican. Baadaye viongozi hao, wamegusia
pia masuala mbali mbali ya kimataifa.