2013-10-26 13:46:24

Papa Francisko ana wazo la kutembelea Argentina, Cile na Uruguay, ifikapo mwaka 2016!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2013 amekutana na kuzungumza na kikundi cha wanafunzi walisoma katika shule za Wayesuit kutoka Uruguay. Wanafunzi hao wa zamani ambao walikuwa na wameandamana na familia zao, wamepongezwa na Baba Mtakatifu kwa kuonesha matumaini mintarafu kumbu kumbu za maisha yake na Uruguay.

Baba Mtakatifu anasema, hadi sasa hakuna ratiba maalum inayoonesha kwamba, angeweza kutembelea nchini Uruguay, lakini ana matumaini kwamba, pengine kunako mwaka 2016, anaweza kutembelea Uruguay, Chile na Argentina, mahali anakota. Baba Mtakatifu amewaomba wanafunzi hao wa zamani kuendelea kumkumbuka katika maisha na utume wake kwa njia ya sala. Anasema, anaendelea kuonja ukarimu na upendo kutoka kwa waamini na watu wenye mapenzi mema wanaofika mjini Vatican kila siku.

Amewapongeza pia wasaidizi wake wa karibu wanaomsaidia kutekeleza wajibu wake kwani hawa ni wenza anaowategemea kwa kiasi kikubwa. Anakiri kwamba, utume wake ni mkubwa na kwamba, ana kazi nyingi za kufanya, jambo la msingi ni kuendelea kuwasindikiza yeye pamoja na wasaidizi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ari na moyo mkuu!







All the contents on this site are copyrighted ©.