2013-10-26 14:14:35

Askofu msaidizi Anastacio Kahango ang'atuka kutoka madarakani; Monsinyo Aldo Giordano ateuliwa kuwa Balozi mpya Bolvia na Venezuela


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Oktoba 2013 amekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu msaidizi Anastacio Kahango wa Jimbo kuu la Luanda, Angola mintarafu sheria za Kanisa namba 411 na 401ยง 1 za Sheria za Kanisa.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Aldo Giordano kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Bolvia na Venezuela na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Mteule Giordano alikuwa ni m wakilishi maalum wa Vatican kwenye Umoja wa Ulaya. Alizaliwa tarehe 20 Agosti 1954 mjini Cuneo, Italia.

Baada ya majiundo na malezi yake ya Kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 28 Julai 1979. Askofu mkuu mteule anauzoefu mkubwa katika taaluma kama Jaalimu la Falsafa. Amekwisha wahi kuteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya kwa takribani miaka 13.







All the contents on this site are copyrighted ©.