2013-10-25 16:18:44

Nafasi ya wanawake katika kulinda na kutetea uhai, utu, heshima na mafao ya wengi!


Shirikisho la Wanawake Wakatoliki Duniani, WUCWO, hivi karibuni lilifungua mkutano wake mkuu kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Fouad Twal, Patriaki wa Yerusalem. Mkutano huu unajadili pamoja na mambo mengine kuhusu zawadi ya uhai, utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu pamoja na mafao ya wengi.

Baadhi ya Wanawake Wakatoliki wanaoshiriki kikamilifu katika masuala ya kisiasa na kijamii huko Mashariki ya Kati wameshirikisha uzoefu na mang'amuzi yao kuhusu mchango wa wanawake katika kudumisha misingi ya haki, amani na upatanisho wa kweli. Wajumbe pia wamegusia dhamana na nafasi ya Bikira Maria kadiri ya Maandiko Matakatifu. Shirikisho hili linatarajia kufunga mkutano wake rasmi, Jumapili ijayo, tarehe 27 Oktoba 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.