Kila mwaka tarehe 24 Oktoba, ni Siku ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa Katibu Mkuu wa
umoja huo, Bwana Ban Ki Moon, kwa ajili ya maadhimisho haya amesema, siku hii inalenga
kutoa utambuzi zaidi, jinsi gani chombo hiki cha thamani sana, hutoa mchango mkubwa
katika udumishaji amani na maendeleo ya wakazi wote wa dunia. Na kwamba , siku hiii
iliwekwa kama fursa ya kutafakari zaidi mipango kwa ajili ya mafanikio na maisha
bora kwa siku za usoni. Aidha katika ujumbe huo, ameitazama hali ya vita na mapigano
yanayoendelea Syria akisema ni changamoto kubwa katika usalama na utulivu wa dunia,
kwa wakati huu, mamillioni ya watu, kuishi kwa kutegemea msaada wa ubinadamu, kuokoa
maisha yao. Ban Ki moon ameonyesha kutambua juhudi za Watalaam wa umoja wa Mataifa
wanao fanyakazi bega kwa bega na Shirika liloshinda Tuzo ya Heshima katika juhudi
za kuzuia silaha za kemikali, ambao wanafanyakazi ya kuangamiza shehena ya kemikali
hizo za hatari zilizo hifadhiwa Syria. Na kwamba, Umoja wa Mataifa unafanya pia jitihada
kupitia msukumo wa kidiplomasia kufikisha mwisho wa kipindi kirefu cha mateso kwa
watu wa Syria. Ujumbe wa Katibu Mkuu, pia umezitaja changamoto zinazo pambana
na ufanikishaji malengo ya Maendeleo na ustawi wa jamii, ukionyesha kutambua kwamba,
umaskini umeweza kupunguzwa kwa nusu. Na kwa sasa kazi kubwa ni kudumisha msukumo
na mshikamano huo katika ufanikishaji wa malengo ya Mandeleo yanayokamilika mwaka
2015, na pia kufikia makubaliano thabiti katika agenda ya kukabiliana na Mabadiliko
ya tabia nchi . Aidha amesema, kwa mara ingine tena mwaka huu, kumeshuhudiwa
Umoja wa Mataifa ukijumuika pamoja kuzungumzia juu ya mizozo ya kutumia silaha, haki
za binadamu , mazingira na masuala mengine . Na Umoja unaendelea kuonyesha kinacho
takiwa zaidi ni ushirikiano , na unawezo wa kutenda zaidi, katika dunia ya leo, iliyounganishwa
zaidi na yenye kuwa na lazima ya kushikamana zaidi. Katibu Mkuu Ban Ki Moon amemalizia
ujumbe wake na wito kwamba, katika Siku hii ya Umoja wa Mataifa , na tutoe ahadi
ya kuyaishi mawazo yetu na kufanya kazi kwa pamoja, kwa ajili ya kufanikisha amani,
Maendeleo na haki za binadamu.