2013-10-22 10:13:16

Tanzia: Askofu mstaafu Bernardo Felipe Governo amefariki dunia!


Askofu mstaafu Bernardo Felipe Governo wa Jimbo Katoliki Quelimane nchini Msumbiji amefariki dunia, Jumapili tarehe 20 Oktoba 2013. Marehemu Askofu Governo alizaliwa tarehe 21 Januari 1939 mjini Macuse, Jimbo Katoliki la Quelimane. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 4 Oktoba 1969. Tarehe 31 Mei 1976 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Quelimane. Tarehe 10 Machi 2007 akang'atuka kutoka madarakani.







All the contents on this site are copyrighted ©.