Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anawaambia
waamini kwamba, ikiwa kama wanataka kumfahamu Kristo wanapaswa kwanza kabisa kujenga
uhusiano wa karibu kwa: kumsikiliza kwa makini katika hali ya ukimya mbele ya Tabernakulo
pamoja na kupokea Sakramenti mbali mbali za Kanisa.