2013-10-21 14:18:47

Balozi Hackett wa Marekani awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 21 Oktoba 2013 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Kenneth Francis Hackett, Balozi mpya wa Marekani mjini Vatican. Alizaliwa tarehe 27 Januari 1947, ameoa na ana watoto wawili. Ni balozi ambaye ana uzoefu na masuala ya Kanisa kwani tangu mwaka 1972 hadi mwaka 2012 amekuwa ni mfanyakazi wa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Marekani.

Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Makamu wa Rais Shirikisho la Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis. Kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2010 alikuwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Challenge. Na kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 2012 alikuwa pia ni mjumbe wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum.







All the contents on this site are copyrighted ©.