2013-10-19 15:28:06

Tutumie vyema utajiri wa miito Afrika


Je sisi ni Wamisionari wa maneno tu maisha yetu yakiwa mbali na Ukristo? Na je ni upi ushuhuda wetu? Ama sisi ni maneno tu lakini tunaishi kama wapagani ? Ni maswali ya Papa Francisko, wakati akitoa Kattekesi yake kwa mahujaji na wageni, Jumatano iliyopita, katekesi iliyo toa mwangwi kwa Siku ya Kimissionari Duniani. Papa alitoa wito kwa waamini wote, kufungua mioyo yao katika mahitaji ya utume na dalili zinazotafuta kujenga mshikamano katika msaada wa kudumisha Makanisa ya mapya.
Mwana habari wa Vatican Roberta Gisotti, katika mwelekeo wa huo, alitaka kujua zaidi juu ya kazi za Uinjilishaji na Utume kwa Bara la Afrika, na hivyo alifanya mahojiano na Askofu Mkuu Protase Rugambwa , Katibu Mwambata katika Shirika la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Kazi za Kipapa za Kitume. Roberta alitaka kujua, iwapo Afrika pia kuna ubutu wa kuitikia mwaliko huu wa Papa.
Askofu Mkuu Rigambwa alijibu swali hilo akisema, kweli mwaliko wa Papa ni muhimu sana , hasa kwa makanisa machanga, yanayoendelea kukua hata katika miito , ili yaweze hatimaye kupata nguvu za uwepo wa Kanisa, Kanisa moja na kitume. Kanisa la kimisionari linalotoka nje kwenda kuhibiri habari Njema ya Injili. Hivyo, kama Wakristo barani Afrika, katika mtazamo wa kimisionari wanaendelea kukua, na kwa bahati kuna miito mingi ... Lakini pia ni lazima kuwa waangalifu , kutotengeneza Kanisa la Kiafrika, ila kuendelea kuwa Kanisa la Ulimwengu, katika maana kwamba ,uwepo wa Kanisa linalokua, pia ni muhimu kutazama mahitaji ya nje ya nchi na nje ya mipaka ya Afrika.

Pia akijibu swali iwapo ni haki kwa makanisa yaliyomo katika nchi tajiri zilizoendelea za Magharibi kuendelea kutoa msaada kwa makanisa machanga, alisema, bila shaka tunazungumzia ushirikiano wa kimisionari. Tunapozungumzia makanisa machanga, tunamshukuru Mungu, kwa waamini wengi kuitikia wito wa Upadre na maisha yaliyowekwa wakfu. Hivyo tunaiona kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, pengine inayolitaka kanisa barani Afrika, pia kupeleka watumishi wa Mungu nje ya Afrika, kama ilivyokuwa wakati Makanisa ya Ulaya yakiwa na miito mingi yalipeleka Mapadre na watawa wengi katika makanisa ya nje .

Hivyo, kwa wakati huu Afrika ikiwa na miito mingi , inakuwa ni wakati wake wa kufungua macho na kuona wapi msaada wa unahitajika, msaada wa kichungaji wa Mapadre na watawa kutoka Afrika, kwenda hnje ya Afrika , kufanya kazi hii muhimuya huduma za Kichungaji, kaziya uinjlishaji . Na hakuna hofu katika hili kwa kuwa kuna maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kazi hii ya utume. Na hivyo hili linaonyesha hata uhalali wa dira ya ushirikiano wa kimisioni katika kanisa moja la kitume.

Askofu Mkuu Rugambwa pia alisisitiza kwamba wana wa Afrika , wanahitaji kujua na kuelewa kwamba hata katika mambo madogo, ushiriki wao ni wa lazima, kushirikiana katika ombi hili la kimisionari, la kila mwaka. Na wanapaswa kutambua umuhimu wa kushirikiana na Baba Mtakatifu, katika juhudi za ufanikishaji wa kazi za kichungaji katika makanisa yote ulimwenguni.
Na hivyo , daima ni lazima kila muumini kuwa mtu wa imani aliye tayari kushiriki katika kazi za misioni kwa kushirikiana na mawakala wote wa kichungaji , ili kazi ya uinjilishaji iendelea kushamiri katika maeneo yote ya dunia.








All the contents on this site are copyrighted ©.