Papa akutana na Tume ya Kimataifa kwa ajili ya kitabu cha Liturujia katika lugha ya
Kiingereza.
(Vatican Radio) Papa Francisko Ijumaa ya 18 .10.13, alikutana na wajumbe wa Tume ya
Kimataifa wanaoshughulika na kutafasiri Liturujia katika lugha ya Kiingereza(ICEL).
Aliwaambia kwamba, matunda ya kazi yao imesaidia kuunda sala za maombi kwa Wakatoliki
wengi.Wajumbe wa ICEL, walikutana Rome kwa lengo la kusherehekea maadhimisho ya miaka
hamisini tangu kuanzishwa kwa tume hiyo. Papa katika hotuba yake kwa wahudumu
na wajumbe wa ICEL, ilianza kwa kutoa shukurani kwa Askofu Mkuu Arthur Roche , Katibu
wa Shirika kwa ajili ya Ibada Takatifu na Nidhamu za Sakramenti , na Rais wa zamani
wa ICEL . Na kupitia kwao Papa alipeleka salaam zake za matashi mema na shukurani
kwa kwa Mabaraza ya Maaskofu waliyoyawakilisha na kwa washauri na wafanyakazi ambao
hushirikiana nao katika kufanikisha kazi za Tume.
Tume hii ilianzishwa kama
sehemu ya utekelezaji wa upya na mabadiliko makubwa katika mfumo wa liturujia kama
ilivyotajwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, juu ya Liturujia Mungu. Kuundwa
kwa ICEL pia ikawa ni moja ya ishara ya roho ya umoja wa Maaskofu, katika upatikanaji
wa Katiba mpya ya Baraza, juu ya Kanuni Sadikifu za Kanisa (taz. . Lumen Gentium
, 22-25 ). Papa aliendelea kueleza kuwa maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuundwa
kwa tume hiyo , ni ishara ya kumshukuru Mungu kwa kazi zilizofanikishwa na Tume katika
kipindi hiki cha miaka hamsini katika kutoa taratibu za Liturujia katika lugha ya
Kiingereza, lakini pia katika kuendeleza utafiti , uelewa na matumizi ya utajiri
wa Kanisa kisakramenti na milaza mapokeo. Lydia O’Kane akiripoti juu ya ICEL,
anasema, Kazi ya Tume pia zimetoa mchango mkubwa katika dhamira , utendaji na ucha
Mungu , kama ilivyotakiwa na Baraza la Mtaguso Mkuu wa Pili , na kama Papa Benedict
XVI alivyowakumbusha mara kwa mara, umuhimu wa kueleweka kwa undani zaidi katika
misingi ya kuelewa siri ya fumbo la Ekaristi linaloadhishwa na mahusiano yake na
maisha ya kila siku "( Sacramentum Caritatis , 52) . Papa Francisko aliwambia wajumbe
wa ICEL kwamba, matunda ya kazi yako si tu yamesaidia wakatoliki kuweza kuunda maombi
ya Wakatoliki mazuri zaidi , lakini pia Imechangia uelewa wa imani , kazi za kawaida
za Padre, na moyo mpya katika utendaji wa utume wa Kanisa kwa kila muumini, kulingana
na mafundisho ya Mtaguso. Kama Mwenye Heri Yohane Paulo II alivyosema, "watu wengi
wameupokea ujumbe wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican,hasa kupitia mageuzi ya kiliturujia
" ( Vicesimus Quintus Annus , 12).
Papa Francisko aliendelea kuishukuru Tume
ya ICEL, kwa kuwezesha idadi kubwa ya waamini wa Kanisa Katoliki Duniani kote kuomba
katika lugha yao mahalia, na pia katika kukuza umoja wa Kanisa katika imani na ushirika
katika sakramenti, ambayo ina asili yake ni katika Utatu Mtakatifu Uliobarikiwa,
ambao daima hupatanisha na kuongeza maana ya utajiri wa utofauti. Papa Francisko
alionyesha tumaini lake kwamba, juhudi zao katika kutafasiri zitaendelea kuwa msaada
wa kuelta ufahamu zaidi kama alivyohimiza Papa Paulo VI katika kueneza imani kupitia
Misale , kwamba, licha ya utofauti mkubwa wa lugha, sala inabaki kuwa ni hiyohiyo
moja, inayotolewa kama sadaka ya kukubalika kwa Baba yetu wa mbinguni , kwa njia ya
juu Kuhani wetu Mkuu Yesu Kristo na katika Roho Mtakatifu. Papa Franisko alimalizia
na kuwapa baraka zake za kitume kwa kazi yao muhimu.