2013-10-18 15:17:21

Papa Francisko na wasaidizi wake watakuwa na mafungo kiroho ya Kwaresima -Albano


(Vatican Radio) Papa Francisko, ameamua, wiki moja ya mafungo ya Kiroho ya kipindi cha Kwaresima kwake yeye na wafanyakazi katika ofisi za Curia ya Roma, kufanyika nyumba ya "Casa del divino Maestro" ya Albano, ambayo ni nyumba ya Watawa wa Mtakatifu Paulo.
Katika mafungo hayo, tafakari za Kiroho,zitaongozwa na Padre wa Jimbo la Roma, Mons. Angelo De Donatis, kuanzia Jumapili jioni ya Machi 9, 2014 hadi Ijumaa asubuhi (14 Machi), ambalo ni wiki ya kwanza ya Kwaresima.

Kulingana na taarifa, lengo ni kwenda kufanya mafungo nje ya Vatican ni kupata mahali pa utulivu na ukimya zaidi, mbali na maeneo ya kazi za kila siku.








All the contents on this site are copyrighted ©.