2013-10-18 16:23:11

Kanisa haliwezi kusahau kuenzi wanaotoa huduma katika nyumba za wazee- Papa


Papa Francisko amesema, kanisa haliwezi kuwasahau Mapadre na Watawa wanaoishi na kuhudumia katika nyumba za wazee,ambazo ni Madhabahu za utakatifu.
Ni ujumbe wa Papa Francisko katika homilia yake ya wakati wa Ibada ya Misa ya mapema asubuhi Ijumaa, aliyo iongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican. Tafakariyake ililenga zaidi kwa Nabii Musa , Yohana Mbatizaji na Mtakatifu Paulo. Alisema, kila mmoja wao, alikuwa na sifa za kutaka kujiepusha na dhiki, lakini Bwana kamwe hakuwa telekeza.

Papa alieleza na kufikiri juu ya Mapadre na Watawa wengi, wanaoishi katika nyumba za wazee na nyumba ya uuguzi, nyumba za wagonjwa ambao kwa uaminifu, wameitikia wito wa kutembea na watu walio katika hali za mwisho mwisho wa maisha, wangi wao wakionekana kuzongwa na ukiwa na kukata tamaa ya kuendelea kuishi, kutokana umri, au maradhi, makazi ambayo kweli ni utume katika madhabahu ya Matakatifu na ya kitume.

Kisha Papa alielekeza katika maisha ya mwanzo ya kitume ya Mtume Paulo na hatima yake. alizitazama pande mbili za maisha ya Mkristu ,ujana na uzeeni , akiona kuwa hata maisha ya mitume, huanzia katika umri wa ujana, wenye nguvu , katika kupambana na vishindo vya mapepo na majaribu ya shetani na wengi walisonga mbele katika mahubiri kwa ujasiri .
Aliwarejea mitume watatu, Musa, Yohana Mbatizaji na Paulo. Musa aliye ongoza taifa la Mungu, kwa ujasiri na mapigano dhidi ya maadui na pia aliyehojiana pia Mungu kwa ajili ya wokovu wa watu, lakini mwisho wake safari yake ngumu, alipofika juu ya Mlima Nebo , na kuangalia nchi ya ahadi, mwili ukiwa umedhoofika na hakuweza kuingia katika ahadi. Nae Yohana Mbatizaji, katika siku zake za mwisho hakuepushwa na huzuni, alizongwa uchungu wa mashaka na mateso, hadi kuagushwa chini na kwa mamlaka ya kiongozi dhaifu, chini ya nguvu ya mzizi mwenye mzizi wa wivu mbele ya mneguaji. Na hata Mtume Paulo katika barua yake ya kwanza, inawazungumzia wale , walio mtelekeza , na wale walioponda mahubiri yake, hakuna aliye jitokeza kumtettea hahakamani, mbele ya mauti wote walitengana nae. Lakini Mtakatifu Paulo alionyesha imani yake kwamba Bwana anamsimamia , na aliendelea kumpa guvu na ujasiri kupitia utangazaji wa Injili, hadi kufikwa na kifo.

Papa ametafakari juhudi za mitume hawa, walio yatolea maisha yao kwa Bwana kwa ajili ya kupata ukomavu zaidi , kama alivyossema Yohane mbatizaji , ni muhimu kwamba, kwa kadri imani yangu inavyozidi kukama ndani ya Moyo wangu ndivyo ninavyojiona kuwa mdhaifu asiyejua kitu. Na pia kwa ahadi iliyotolewa kwa Petro, kwamba, wakati utakapokuwa na umri mkubwa watamchukua mahali ambapo asipotaka kwenda .

Kwa fikara hizo, Papa aliwakumbuka ndani ya moyo wake wale wote wanaoishi katika vituo vya wazee, ambavyo ameviita kuwa ni madhabahu za utakatifu ,akiwataja Mapadre na watawa wanao toa huduma katika vituo hivyo vya watu wenye umri mkubwa, watu waliozongwa na upweke , wakisubiri Bwana kuja kugonga kwenye mlango wa mioyo yao . Haya ni madhabahu ya kweli ya mtiririko wa kitume na utakatifu, ambayo hayawezi kusahauliwa na kanisa. Papa alieleza na kutazamisha katika madhabahu mbalimbali za Kanisa , za Mama Bikira Maria, Mtakatifu Francisko, Mtakatifu Benedikto na nyingine nyingi.


Sisi wote ,alihitimisha Papa, tunapaswa kufikiria kuhusu hatua hii ya maisha, machweo ya utume na kuomba kwa Bwana, tukisema Ndiyo, Bwana, mimi nataka kukufuata wewe ulipo.







All the contents on this site are copyrighted ©.