Tasisi ya Mo Ibrahim juu ya Utawala Bora Afrika, imebaini nchi za Rwanda na Tanzania
kuwa nchi zenye utawala bora zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya
nchi 52 za kiafrika. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatatu tarehe 14 Oktoba 2013,
Rwanda imepata wastani wa asilimia 57.8 ikiwa ni zaidi ya wastani wa kiafrika wa asilimia
51.6.
Hii inamaanisha kwamba nchi hiyo imeboresha utawala bora kwa zaidi ya
asilimia 10.9 tangu mwaka 2000, ikiwa nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki
ikifuatiwa na Tanzania iliyoshika nafasi ya 17 Barani Afrika kwa kupata asilimia 56.9
huku Uganda ikiwa ya tatu EAC kwa kuwa ya 18 kwa kupata asilimia 56. Kenya imekuwa
ya 21 na kushika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 53.6 huku Burundi iliyopata asilimia
43.8 ikishika nafasi tano kwa EAC.
''Rwanda imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi
mwaka kuanzia mwaka 2000, ikiwa ni maboresho makubwa zaidi katika nyanja ya Maendeleo
ya Binadamu hususa ni katika sekta ya elimu na afya,'' ripote ilisema. Mauritania
imeshika nafasi ya kwanza katika Afrika kwa kupata asilimia 82.9 ikifuatiwa na Botswana
aliyopata asilimia 77.6 ambapo Cape Verde imeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia
76.7. Barani.
Ripoti hiyo imebaini kwamba asilimia 94 ya nchi za Afrika ikiwemo
Rwanda watu wake wanaishi katika nchi ambazo zimeboresha kwa ujumla masuala ya utawala
bora tangu mwaka 2000. Asilimia sita ya watu wanaoishi kwenye nchi ambazo kiwango
cha utawala bora kimeshuka tangu mwaka 2000 ni pamoja na nchi za Guinea-Bissau, Madagascar,
Somalia, Libya na Mali.
Taasisi hiyo ya Mo Ibrahim pia hutoa tuzo kwa viongozi
bora barani Afrika.Hata hivyo tuzo hiyo haijatolewa kwa mara ya nne sasa. Tuzo hiyo
hotolewa kwa kiongozi wa Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia aliyeonesha kwa vitendo
uongozi bora,kutumikia muhula wake wa uongozi na kuachia ngazi miaka mitatu iliyopita.