2013-10-17 11:28:10

Sala ya Mwaka wa Imani, Jimbo kuu la Nairobi


Ee Mungu Baba Mwenyezi Mwenyezi, tunakushukuru kwa zawadi ya imani na ya kila mmoja wetu. Tunakuomba ili Wakristo Jimbo kuu la Nairobi, wajaliwe kukufahamu na kukupenda wewe; wakue na kukomaa katika ufuasi wa Mwanao Yesu Kristo; wawe washiriki hai wa maisha na utume wa Kanisa; tutumie karama zetu kujenga Ufalme wa Mungu na Wokovu wa roho za watu.

Tuombe, Njoo Roho Mtakatifu, uieneze mioyo ya waamini wako; washa moto wa mapendo, vitaumbwa upya na sura ya nchi itageuka. Ee Mungu Baba Mwenyezi ambaye ulifundisha mioyo ya waamini wako, utujalie mwanga wa Roho Mtakatifu. Ili tuweze kuwa na hekima pamoja na kufurahia faraja yake. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.