2013-10-15 15:05:10

Uteuzi wa Papa:


Papa Francescisko amemteua Kardinali Peter Erdo, Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest, kuwa Msimamizi Mkuu wa Sinodi Maalum ya Maaskofu, itakayofayika 5-19 Oktoba 2014, juu ya "Changamoto za Familia katika mtazamo wa Uinjilishaji mpya". Pia kwa ajili hiyo, Papa amemteua kuwa Katibu Mkuu wa sinodi hiyo, Askofu Mkuu wa Bruno Forte, wa Jimbo Kuu la Chieti-Vasto.
Jimbo la Uvira lapata Askofu mpya
Baba Mtakatifu Francisko , Jumanne 15 Octoba 2013, amemteua kuwa Askofu wa Jimbo la Uvira Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, Monsiyori Sèbastien Muyengo Mulombe. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni AskofuMsaidizi wa Jimbo Kuu la Kinshasa.
Kapanda Cheo
Padre Fernando Vèrgez Alzaga , kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa utawala katika nchi ya Vatican, Baba Mtakatifu amempandisha cheo na kuwa Askofu wa Jina wa Villamagna di Proconsolare.










All the contents on this site are copyrighted ©.