Papa aonya dhidi ya ucha Mungu, usiokuwa na huruma au kujali wahitaji maskini.
(Vatican Radio) Jumatatu Papa akifafanua juu ya Ishara ya Yona iliyoelezwa katika
Injili ya Luka, alionya juu ya tabia ya kuwa mcha Mungu kamili, lakini asiyejali
wahitaji na maskini. Papa alionya dhidi ya tabia hiyo , wakati wa Ibada ya Misa mapema
Jumatatu, aliyoiongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican. Papa
alirejea somo la Injili lililo somwa Jumatatu, ambamo mlizungumziwa Ishara ya Yona,
na Yesu anazungumza juu ya kizazi kiovu kwamba, Yesu kwa maneno hayo, hakuwalenga
wale waliokuwa wakimfuata kwa roho ya kweli na upendo kamili, lakini aliwalenga zaidi
wanafiki walimu mafarisayo, ambao waliolenga kumjaribu na kumfanya aanguke katika
mtego,katika kuyajibu maswali yao.
Papa Francis aliendelea kueleza kuwa,
Mafarisayo kw aunafiki walimwuliza Yesu, na Yesu kwa kujua hila yao, aliwajibu kuwa
ni yeye peke atakayekuwa Ishara ya Yona, kama Yona mwenyewe alivyokuwa ishara kwa
Waninawi .
Baba Mtakatifu alisema kwamba, watu hao walikuwa wakiteswa na kile
kinachoitwa “ishara ya Yona" na Yesu anawaita wanafiki kwa sababu wana "walionekana
kuyajua mafundisho ya dini yanavyosema na kuyatii , lakini ndani ya mioyo yao hwakuwa
na upendo kwa watu wengine, na hasa katika kuwajali wahitaji maskini.
Papa
aliendelea kwa kusema kwamba " Ishara ya Yona ", ni ishara ya ukweli yenye kutupatia
sisi uhakika wa matumaini kuokolewa kwa damu ya Kristo. Papa alisisitiza kwa kuuliza
ni Wakristu wagapi wanaofikiria wataokolewa kwa utume wao?Alitoa jibu , ni kweli kazi
ni muhimu, lakini kazi ni matokeo ya utoaji wa jibu la upendo wa huruma uliotuokoa
sisi . Kazi isiyoandamana na matendo ya huruma na upendo wa kina, utendaji huo ni
bure. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Ishara ya Yona, ni sawa na kazi bila upendo na huruma.
Papa alimalizia kwa kusema kwamba tunapaswa kuchukua faida ya Liturujia
ya Jumatatu, kujichunguza sisi wenyewe na kutoa jibu sahihi, je mimi nina fanya kile
ninachopendelea zaidi, au utendaji wangu ni “ Ishara ya Yona”?