Jifunueni katika umoja na mshikamano wa binadamu wote-Kardinali Tarcisio Bertone.
Jumapili Oktoba 13 2013, wakati Papa Francisko akiongoza Ibada ya Misa katika Kuu
la Mtakatifu Petro na kuikabidhi dunia chini ya Moyo Mtakatifu sana wa Bikira Maria,
nae Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu wa Nchi ya Vatican, na Jimbo Takatifu kwa
ujumla, aliongoza Ibada ya Ekaristi katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Fatima.
Taarifa
inaeleza Jumamosi 12 Oktoba, Kardinali Tarcisio aliongoza maadhimisho ya kumbukumbu
ya kupita miaka sitini ya Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Rozari,alilo litaja kuwa ni
Nyumba ya Mama, ambamo mahujaji hukusanyika kwa lengo la kukutana na Mwanae Yesu
Kristu, anayewaalika katika njia ya uongofu, maisha ya kutembea katika njia isiyo
ya udanganyifu , ila njia inayongoza katika utulivu kamili wa maisha si ya kiroho
tu lakini hata kimwili. Ni kama ilivyokuwa kwa Zakayo aliyeketi kwa utulivu juu ya
matawi ya mkuyu ili apate kumwona Kristo akipita na kuwa kinyume chake, Bwana anapofikia,
alimwita zakayo na kumtaka ateremke haraka maana alipenda kula chakula katika nyumba
yake. Kardinali alisema , nasi licha ya mahali tupo na tulivyo, tunaitwa kuteremka
hima kutoka katika starehe za dhambi na kukutana na Yesu, anayetaka kula chakula pamoja
nasi katika mioyo yetu, nyumba zetu na familia zetu. Kardinali aliendelea kusema,
Yesu, aliwapokea wote kama ndugu , wema wenye dhambi, wanafiki na watoza ushuru.
Mwinjilisti Luka , kwa kweli, anatoa changamoto kwetu, kuvunja kuta za utengano
kati ya wale wanaofikiri ni wema na wale wenye dhambi. Na kwamba huu ni mwaliko
kwa wote wanaofika katika madhabahu hayo, ili kwamba, tokea hapo, wote wawe wamemeitikia
mwaliko wa kushirikiana na umoja watu wote kama mawe hai ya msingi, yakiinua moja
kwa jingine, kusaidia kuidumisha nyumba ya Mungu yaani Kanisa, na ujenzi wa misingi
ya maisha ya Kikristu kwa watu wote. Aliongeza, kwamba, hata katika hali za umasikini,
kanisa linapaswa kuendelea na utume huu wa kuishi kwa upendo na shikamano, na hasa
katika kuihubiri habari njema kwa watu wote, matajiri, maskini na wanyonge. Kardinali
Tarcisio, akihitimisha maadhimisho ya Siku Kuu ya Mama Yetu wa Fatima, pia alitaja
jinsi maisha yetu yanavyoishi katika hali za vitisho na udhaifu na hatari nyingine
zinazo jitokeza katika uzoefu wa maisha ya kutokuwa na uwezo wa kuyatawala ya usoni
tusiyoyajua, hofu kwa madhulumu na maut. Lakini akasisitiza kwamba, tuna neno la
mwisho juu ya uwepo wa binadamu, ambalo ni matumaini ya kweli katika kupata ushindi
juu ya dhambi na mauti na changamoto za maisha. Neno lenye kutoa ujasiri na maamuzi
ya kutaka kuuona uso wa Mungu, katika maisha yetu. Neno la Injili ya kuokoa inayongoza
katika maisha ya milele yasiyokuwa na wasiwasi na hofu.
Kardinali alitaja
kiini cha ujumbe wa Tukio la Mama Yetu Fatima kwamba , ni uongofu kwa Mungu, kanuni
inayorejesha upya jamii ya binadamu wote kwa Mungu. Matukio ya Maria kuwatokea kwa
mara kadhaa watoto wa Fatima, ni mwaliko unao tutaka tujibidishe katika juhudi za
kutaka kuuona uso wa Yesu. Ubinadamu wetu wote ni pamoja na Maria, katika uhakika
kwamba, upendo huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, alieleza Kardinali
Tarcisio. Kama sisi tunaishi katika umoja na Mungu , kwa njia ya Maria hofu huteketea,
kama mandhari ya kichungaji iliyoandikwa katika madhabahu hayo inavyosema : " Usiogope
".