Wakristu ,igeni maisha ya wafia dini-Papa Francisko
Papa Francisko ametoa wito kwa Wakristu, kuwaiga mashahidi wafia dini ili kuondokana
na hali ya kuwa wakristu bandia. Papa alitoa wito huo, siku ya Jumapili, kwa njia
ya video , katika ujumbe wake, kwa ajili ya tukio la kihistoria la kutajwa kuwa Wenye
Heri, mashahidi wafia dini 522 , Wahispania, waliouawa wakati wa adha ya mapambano
dhidi ya Ukristo katika ya miaka ya 1930.
Katika ujumbe huu, Papa ameonyesha
ukaribu wake katika sherehe hizi zilizofanyika Tarragona, Hispania , ambako idadi
kubwa ya Mapadre, ,na watawa, na walei aminifu katika imani , walitangazwa kuwa Wenye
Heri Mashahidi wa Imani, Jumapili iliyopita. .
Hotuba hiyo fupi ya Papa kwa
ajili ya tukio hilo, amewatazama kwa makini sana, mashahidi hao na kusema kwamba,
hawa walikuwa ni Wakristo wa kawaida, lakini waliishi kwa uaminifu, katika kuifuata
njia ya Kristo. Ni wanafunzi wa Yesu waliojifunza vyema anachokitaka Bwana wao, kwamba
ni upendo wa hali ya juu kwa Kristu, kama Yeye Yesu alivyotembea katika njia hiyo
hadi mauti msalabani kwa ajili ya utukufu wake Mungu.
Papa akiuelezea upendo
huo anasema, haukuwa upendo nusunusu, au uliotolewa kwa vipindivipindi bali ni ulikuwa
ni upendo kamili. Ni upendo unaokwenda hadi miisho ya maisha, juu ya msalaba. Pamoja
na Yesu kuusikia uzito wa mauti , uzito wa dhambi za binadamu, hakusita kuitoa nafsi
yake nzima kwa Baba, kwa ajili ya kumkomboa binadamu, na mzigo huo wa dhambi. Akiwa
msalabani Yesu alitoa maneno machache, lakini muhimu, yaliyo toa zawadi ya maisha.
hili linaonyesha wazi kwamba, Kristo anatupenda kwa upendo usiokuwa na kiasi. Na
ndivyo wafuasi wake Mashahidi wafia dini waliotajwa kuwa Wenye Heri, waliuishi upendo
huo mpaka mwisho wa maisha yao.
Papa alihimiza waamini kuyaiga maisha ya wafiadini
hawa. Na kwamba ni lazima daima kufa kwa ajili ya kujitakatifusha wenyewe, dhidi
ya binafsi wetu, ustawi , uvivu wetu, majonzi yetu, na kujifunua kwa Mungu,na
kwa wengine , hasa wale wanao tuhitaji zaidi.
Papa aliendelea kuomba maombezi
ya mashahidi, ili tuwe Wakristo halisi wa kweli, Wakristo katika matendo na si tu
kwa maneno , tusiwe Wakristu vigeugeu lakini thabiti katika upendo wa hali ya juu
kwa usiokuwa butu, hadi mwisho wa maisha. Papa aliomba msaada wao katika kudumisha
imani yetu thabiti , hata wakati wa matatizo yetu, na katika kuboresha matumaini
na kukuza udugu na mshikamano.