Siku kuu ya Mama Yetu wa Fatima: Papa ahimiza waamini kusema "ndiyo" kama Maria.
Jumapili iliyopita 13 Oktoba, ambayo ilikuwa ni Sherehe ya maadhimisho ya Siku Kuu
Mama Yetu Maria wa Fatima , tukio lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka
wa Imani, kwenye kumbukumbuku ya Bikira Maria kuwatokea watoto wa Fatima 13 Oktoba
1917, Sanamu asilia ya Fatima ililetwa Vatican, na kuwekwa katika Uwanja wa Kanisa
Kuu la Mtakatifu Petro, mapema asubuhi kwa ajili ya maadhimisho ya Ibada ya Misa iliyoongozwa
na Papa Francisko. Mara baada ya Ibada, Papa pia, aliiweka wakfu dunia kwa Moyo
Safi wa Maria, Ibada hii ya Misa iliyohudhuriwa na umati wa watu zaidi ya laki moja,
katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro. .
Papa Francisko, akiongoza
Ibada katika uwanja huo, kwenye homilia yake alitaja mambo matatu: Maajabu ya Mungu,
uaminifu kwa Mungu na Mungu ni nguvu yetu." Papa alizungumzia juu ya kweli hizi
tatu, na kuomba msaada wa Maria Mkingiwa dhambi ya asili uzidi kutuongoza katika maisha
yetu ya kila siku. Lakini ili tuweze kupata mafao ya msaada huu, Papa alisema muumini
anahitaji kuwa na maisha adilifu na aminifu katika imani, kutolea shukurani na sifa
Mungu na kumtukuza Kristu aliye nguvu yetu. Papa alieleza kwa kuirejea Zaburi
:” Mwimbieni Bwana wimbo mpya , kwa maana ametenda mambo ya ajabu" ( Zab 98:1 ). Papa
alifafanua leo tunaona moja ya mambo ya ajabu ambayo Bwana amefanya : Maria ! Kiumbe
wa hali ya chini na dhaifu kama sisi wenyewe, lakini yeye alichaguliwa kuwa Mama wa
Mungu , Mama wa Muumba wake.
Papa aliendelea kumtaza Maria kwa makini , na
kutoa mwaliko kwa waumini kutafakari kweli hizo tatu , kulingana na neno lake( Lk
1:38 ), ambamo tunaona kuwa utendaji wa Mungu daima hushangaza, kwa kuwa katika kupungukiwa
, udhaifu na fedhaha ndimo hujionyesha upendo wake wa kutuokoa kutuponya na kutupatia
nguvu. Na anachokiomba ni tu kulitii neno lake na kumwamini. Na hayo ndiyo maisha
aliyo yaishi Bikira Maria . Wakati akipata ujumbe wa Mungu toka kwa Malakia hakuweza
kuficha mshangao wake .Alishangaa kwa jinsi Mungu anaweza kuwa binadamu , kuptia kwake,
yeye aliyekuwa binti maskini wa Nazareth. Mungu hakuchagua binti anayeishi katika
majengo ya kifahari na mwenye mamlaka au utajiri mkubwa, wala aliyekuwa ametenda mambo
makubwa ya kushangaza , lakini anamchangua Maria, anayeishi maisha ya kawaida ambaye
moyo wake umejifunua kwa Mungu kwa unyenyekevu na utii. Maria baada ya kupaswa habari
na Malaika , bila ya kuelewa vyema kila kitu alisema ndiyo kwa mungu , mimi hapa Mtumishi
wake , nitendewe kana unavyonena. Papa anasema, kwa wengi wetu, kuna ugumu kubaki
imara na aminifu katika maamuzi tunayofanya na ahadi tunazo weka. Mara nyingi ni
rahisi kusema "ndiyo" , lakini tunashindwa kurudia "ndiyo" kila siku. Tunashindwa
kuwa waminifu.
Maria akasema "ndiyo yake" kwa Mungu: " ndiyo" ambayo ilibadilisha
maisha yake. Ndiyo aliyoitaja hata wakati wa uchungu na huzuni kuu. Ndiyo katika
kilele cha maisha ya mwanae chini ya Msalaba. Mwanamke mwaminifu , bado amesimama
, chini ya msalaba akiwa amevunjika moyo lakini bado mwaminifu na mwenye nguvu.
Papa
alieleza na kuhoji iwapo sisi kama Wakristu tuna ndiyo hiyo ya kuishi na Mungu nyakati
zote katika furaha, uchungu, mateso na hata mauti. Mungu anatutaka kuwa waaminifu
kwake, kila siku katika maisha yetu ya kila siku . Huruma ya Mungu kamwe haiachi
kuuonyosha mkono wake wa kutuinua sisi juu, kututia nguvu katika safari yetu, na
kutembea pamoja nasi licha ya udhaifu wetu, ili aweze kutupatia nguvu zake. Hii ni
safari halisi: kutembea na Bwana siku zote , hata katika wakati wa udhaifu , hata
katika dhambi zetu. Papa alieleza na kuhimiza waamini kung’ang’ana na jibu la
ndiyo, katika kumfuata Yesu, ahadi waliotoa wakati wa ubatizo. Ni kuzikataa njia zote
zinazotaka kutupeleka nje ya njia ya Yesu, ambazo huua mwili na Roho. Ni kubaki na
jibu la ndiyo , kama ilivyokuwa kwa Maria.
Papa akizungumzia Mungu ni nguvu
yetu . Aliwatazama kwa makini ,watu kumi wenye ukoma walioponywa na Yesu katika
Injili, waliosimama mbali nae na kuita kwa sauti kuu, Yesu Mwalimu, utuhurumie !
(Lk 17:13). Yesu aliwaangalia wagonjwa hao kwa huruma, aliona wanahitaji upendo na
nguvu. Walihitaji kupona, na Yesu kwa upendo na huruma yake akawaponya. Lakini baada
ya kuponywa ni mmoja tu aliyerudi nyuma kutoa asante na kumtukuza Mungu. Yesu anauliza
wengine wamekwenda wapi, mbona ni mmoja tu aliyerudi na kushukuru na kumtukuza Mungu
kwa sauti kubwa na kukiri kwamba yeye ndiye mwenye nguvu iliyomponya?. Papa anasema,
hili ni fundisho kubwa kwa wamini. Alibaini, tunafahamishwa kwamba, ni muhimu kutoa
shukrani , kutoa sifa kwa ajili ya kila kitu Bwana amefanya kwa ajili yetu .
Papa
alieleza na kumrejea tena Maria ambaye baada ya kupashwa habari kwamba atamzaa Yesu,
Masiya Mkombozi wa dunia ,tendo lake la kwanza ni tendo la upendo, kwenda kumtembelea
jamaa yake Elizabeth mzee. Na Maneno yake ya kwanza, ilikuwa " Moyo wangu wamtukuza
Bwana ", kwa maneno mengine, huu ni wimbo wa sifa na shukrani kwa Mungu si tu kwa
kwamba alifanya kwa ajili yake, lakini kwa yale aliyoyatenda katika historia ya wokovu.
Kila jambo na kila kitu ni zawadi toka kwa Mungu . Kama tunaweza kutambua kwamba
kila kitu ni zawadi ya Mungu , jinsi gani ilivyo furaha kwa mioyo yetu! Kila jambo
na kila kitu ni zawadi yake . Yeye ni nguvu yetu! Papa alifundisha na kutahadharisha
kusema " asante" ni jambo kama rahisi, na hivyo bado ngumu! Mara ngapi sisi tunasema
asante mmoja kwa mwingine katika familia zetu? Haya ni maneno muhimu kwa maisha yetu
ya kawaida. Mara ngapi sisi ni kusema asante kwa wale wanao tusaidia au walio karibu
nasi, na wale walio tuunga mkono katika maisha yetu?. Papa anaonya mara nyingi
kuna mwelekeo wa kujisahau na kuona kupewa kitu au kutendewa mema ni haki yetu .
Anasema sawa ni haki yetu lakini pia ni wajibu na tunapaswa kusema asante kwa kila
jambo ! Asante kwa Mungu . Ni rahisi kwa njia ya sala kumwomba Bwana mahitaji yetu,
lakini, tazama jinsi ilivyo rahisi mara tunapojaliwa, kusahau kwenda na kushukuru.
Tunaona hakuna haja, hatuma muda. wakati wa kuomba tulikuwa na muda, lakini muda huo
haupo wakti wa kushukuru ! Papa aliasa na kuhitimisha kwa kuomba msaada wa maombezi
ya Maria, atusaidie kuyaona matendo ya kushangaza ya Mungu , kuwa waaminifu kwake
na kila siku, kumsifu na kumshukuru , kwa kuwa yeye ni nguvu yetu.