Papa aweka wakfu dunia kwa Moyo Mtakatifu sana wa Maria
Jumapili, katika kuhitimisha Ibada ya Misa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu ya
Mama Yetu wa Fatima, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa akiwa mbele
ya sanamu ya Mama Yetu wa Fatima, alitolea heshima na sala, na kuiweka wakfu dunia,
kwa Moyo Mtakatifu sana wa Bikira Maria. Papa aliitazama sana sanamu hiyo na kusema
Asante Mama kwa wale wote walikuja karibu nawe katika Siku Kuu hii na kujiweka chini
ya ulinzi, Msaada wa waumini.