2013-10-12 08:30:36

Miaka 40 ya uwepo wa Kanisa la "Corpus Christi" Kumasi Ghana.


Waumini Wakristo hawana budi kuonyesha upendo na mshikamano ndani ya jami kwa ajili ya mafao ya watu wote wa Mungu. Haya yamesemwa na Padre Thomas Agyemang Prempeh wa kanisa Katoliki la "Corpus Christi" lililoko New Tafo mjini Kumasi.

Padre Agyemang ameyasema haya siku ya Jumapili wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Kanisa hilo. Wakati wa maadhimisho hayo waumini walipata uchunguzi wa bure ili kubainisha hali zao z kiafya kwa ushirikiano wa Kanisa hilo na kikundi cha madaktari kutoka shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la "Project Abroad".

Uchunguzi huo umewasaidia zaidi ya waumini 3,000 wa Kanisa hilo kujua hali zao za kiafya kutokana na magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na Pressure.

Ramsha ramsha zilizoandaliwa kwenye sherehe hizo zilikuwa ni pamoja na michezo kadhaa ya nje na ya ndani kwa ajili ya kuwafurahisha waliohudhuria. Naye paroko wa Kanisa hilo, alichukua fursa ya sherehe hizo kutoa mwito kwa wakristo wa parokia hiyo kuendeleza mshikamano na hasa wa kujenga amani. Padre huyo amesema kuwa nchi ya Ghana haiwezi kuwa na maendeleo ya kudumu pasi na amani ya kweli, na kwamba ni jukumu la kila mwuumini kujenga na kulinda amani hiyo.











All the contents on this site are copyrighted ©.