2013-10-11 16:10:23

Papa atoa msaada wa vocha za simu kwa wahamiaji na wakimbizi Lampedusa


Papa Francisko anendelea kufuatilia na kutoa kipaumbele, kwa hali ya watu wahamiaji na wakimbizi wanaoingia barani Ulaya kupitia Mlango wa kisiwa cha Lampedusa, kabla hawaja sambaa sehemu mbalimbali za Ulaya kujitafutia maisha yaliyo bora zaidi. Jumatano Papa, alipokea ripoti kamili ya Msaada uliotolewa kwa niaba ya Papa, kwa wahitaji wahamiaji na wakimbizi walioingia katika kisiwa cha Lampedusa, ikiwa kimepita kipindi cha wiki moja tangu atoe tamko lake la kusaidia wahitaji hao.
Askofu Mkuu Francisko Montenegro, Askofu Mkuu wa Agrigento, anasema msaada wa Papa , unawafanya wajisikie kwamba Papa yu pamoja nao katika wakati huu mgumu wa majonzi na huzuni kubwa. Na kwamba, msaada wa Papa ni ishara ya kuwakumbatia wote moyoni mwake. Lakini akataja cha muhimu zaidi , ni udumishaji wa msaada wa kiroho na kisaikolojia kwa watu hawa walio shuhudia wenzi wao wakiwa katika mahangaiko ya mwisho ya kukata roho ndani ya maji, watu wenye kuwa na picha ya taabu ya mauti, wakiona wale waliokumbatia rosari takatifu na msalaba, katika utambuzi kwamba mauti yamewakaribia.

Askofu Mkuu huyo anasema, kwa wakati huu bado wanaendelea kutathimini msaada gani zaidi unaweza kutolewa na Papa, ambaye hivi karibuni ametoa msaada wa uliowezesha kununuliwa kwa vocha za simu 1600 zilizo tolewa kwa wahamiaji ili waweze kuendelea kuwasiliana na jamaa zao wa mbali . Na pia msaada wa Papa umewezesha kununuliwa kwa mahema na kuandaa chumba cha mchezo kwa watoto katika kambi hiyo ya Lampedusa. .

Aidha amesema, uopoaji wa miili iliyokuwa imenaswa katika boti waliokuwa wakisafiria iliyozama, hatua hiyo ni kama imemalizika , ingawa bado kuna wazamiaji wanaoendelea kutafuta miili ya watu. Na wakati wa kupiga mbizi za mwisho rasmi watalaam hao katika mbizi, waliweka katika kilele cha mlingoti wa jahazi iliyo zama, taji la Rosari iliyobarikiwa na Papa Francisko.








All the contents on this site are copyrighted ©.