2013-10-11 08:29:45

Papa aomba amani na kuwataka Wakristu na Waislamu waimarishe urafiki na udugu


Papa Fancisko ametoa wito kwa dunia kuomba amani na hasa kwa ajili ya Mashariki ya Kati, akilenga Wakristo na Waislamu waimarishe mapatano, urafiki na udugu.

Papa alitoa rai hiyo siku ya Jumatano , wakati akisalimia makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kusikiliza katekesi yake. Baada ya katekesi, aliwahimiza waendelee kutolea sala na maombi kwa ajili ya amani ulimwenguni kote na hasa Mashariki ya Kati.

Papa alitoa himizo hilo , katika muono kwamba, mwaka mmoja uliopita, Papa Mstaafu Benedict XVI, baada ya safari yake ya Lebanon, aliagiza kuingizwa lugha ya Kiarabu, katika tafasiri za moja kwa moja za katekesi za Papa na maelezo mengine ya jumla, ili ujumbe wa Papa uweze kuwafikia watu wote wa Mashariki ya kati na hasa jumuia za Wkristo Mashariki ya Kati. Pia hatua hiyo inaonyesha ukaribu wa Kanisa Katoliki kwa wanawe wa Mashariki ya Kati. Papa Francesko alikumbusha ni muhimu maelezo pia kutolewa kwa uaminifu katika lugha hii ya Kiarabu.

Papa Francisko alirudia kuhimiza akisema" Ninawaomba msali na kutolea sadaka za maombi na toba, kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati : Syria , Iraq, Misri , Lebanon na Nchi Takatifu, ambapo alizaliwa Mfalme wa Amani , Yesu Kristo. Kuomba kwamba mwanga wa Kristo, umulike katika kila moyo na kila mahali, hata miisho ya dunia “.

Wakati huohuo, Papa aliwakaribisha Maaskofu wanaoshiriki katika Mkutano wa Maaskofu wa Mkoa wa Afrika Kaskazini, na watazamaji,huku akihimiza uimarishaji wa mahusiano ya kidugu pamoja na waamini wa dini ya Kiislamu. Na pia wasisahau kumwomba Roho Mtakatifu ili kwamba kila uso ya mwanaume na mwanamke, daima uwe tayari kutangaza kwa furaha kwa kila mtu na kila mahali, Injili ya wokovu. "

Mwisho, ili moyo ya kila mtu uguswe na majeraha ya Yesu, yanayoonekana zaidi kwa watu dhaifu na masikini wengi. Na kwa namna ya pekee Papa alitoa salaaam zake kwa Kanisa na Maaskofu wa Kanisa la Alexandria la mapokeo ya Ethiopia na Eritrea, ambao kwa wakati huu wako katika maombolezo na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao , waliopotea katiak janaga la boti waliokuwa wakisafiria kuzama maji karibu na kisiwa kidogo cha Lampedusa hivi karibuni .








All the contents on this site are copyrighted ©.