2013-10-09 08:27:50

Yatimia miaka 25 tangu kutolewa hati ya kichungaji juu ya Hadhi ya Wanawake.


Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei limeandaa semina ya siku mbili Oktoba 10-12, kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia miaka 25 tangu kutolewa kwa hati ya Kitume ya Papa Yohane Paulo 11, juu ya heshima na hadhi ya mwanamke, hati inayojulikana kwa jina "Mulieris dignitateM". Hati iliyochapishwa tarehe 15 Agosti 1988.

Madhari ilitakayoongoza semina ni "Ni Mungu aliudhamini ubinadamu kwa mwanamke.Likiwa limepania Baraza hilo linatazamia kwa nguvu zote, na pengine muda hautoshi, kuchabua utekelezaji wa yaliyomo katika hati hiyo, hasa katika miaka ya hivi karibuni.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, lina nia ya kutoa pendekezo katika kutafakari upya juu ya hati hii muhimu, ambayo iliandikwa mwaka 1987, mara baada ya Sinodi ya Maaskofu, iliyojadili Wito na Utume wa walei katika Kanisa na ulimwenguni. Asili yake ni kutoka Sinodi ya Maaskofu, iliyofikiria kwa makini misingi ya jamii katika uadilifu wa kiteolojia na hadhi ya wanawake kama msingi muhimu katika utekelezaji wa kila jambo katika maisha ya Kanisa. .
Hati ya kitume ya Sinodi iliyochapishwa muda mfupi baada ya hati ya Mulieris Dignatatem, ilionya juu ya umuhimu wa wanawake kushirikishwa kikamilifu katika kazi na uwajibika, ndani ya Kanisa katika utekelezaji wa kazi . . ... Kanuni mpya ya sheria za Kanisa, inataja nafasi nyingi zinazoweza kushirikishwa mwanamke licha ya tofauti za a kitamaduni na unyeti fursa ya wachungaji kutekelezwa kwa haraka zaidi azimio hilo.
Semina hii itahudhuriwa na wataalam na wawakilishi wa vyama na jumuiya , kutoka nchi 25 ,ikiwa jumuiya 39 na vyama vya kikanisa , kutoka maeneo tofauti ambao ni mchanganyiko wa wanateolojia, wanafalsafa, waelimishaji, wasomi, waandishi wa habari , wanahistoria , madaktari, wanasheria , wasanii , wahandisi , nk. Ni kundi wanawake na wanaume ambao wataweza kuketi na kuzungumza pamoja, juu ya Kanisa na jinsi Kanisa linavyoweza kushiriki katika changamoto mpya na mwendelezo wa majibu sahihi, katika kuheshimu hadhi ya mwanamke na wito uliotolewa na Mungu kwa kila mwanamke na kila mtu.









All the contents on this site are copyrighted ©.