Msijifungue majumbani bali tokeni mkakutane wa watu-CCEE
Maaskofu wa Ulaya waambiwa "msijifungie katika ngome zenu,tokeni nje mkakutane na
watu kama viongozi wa matumaini". Ni jibu la Kanisa la Ulaya katika kufanya mageuzi
kwenye mamlaka ya Ulaya. Bila kujali nini kinatokea, wakristu wamehimizwa kudumisha
utambulisho wao wazi uliosimikwa katika imani kwamba, imani yao ni hai nyenye kuvuvia
daima mwamko wa tumaini jipya.
Matumaini, ni neno lililo hitimisha Mkutano
wa Marais wa Mabaraza Katoliki Ulaya, (CCEE) Jumapili iliyopita huko Bratislava,
Slovakia. Katika siku hizo za mkutano, Maaskofu wameweza kujadili mada “Mungu na serikali
, Ulaya kati ya watu na Malimwengu", na changamoto katika kuwasilisha tamko la
mwisho iliyotolewa Jumatatu na CCEE. Majadiliano yao yalifuatiwa na mada ya utafiti,
mara kadhaa kwa ajili ya kuimarisha tumaini, imani na uzoefu na maudhui ya kuvutia
kwa kila mtu.
Mara kadhaa , Maaskofu walikiri kwamaba imani katika matumaini,
huliwezesha kanisa kudumu duniani. NI tumaini linalowapa Wakristo, ujasiri wa kukabiliana
na hali ngumu na roho ya uwazi kwa hoja za watu, zaidi ya yote kwanza kabisa ni utume
wa uinjilishaji wa kanisa. Inaendelea CCEE –ni lazima kuwa tayari wakati wote
kuingilia kati katika maamuzi muhimu yanayotolewa na serikali na hivyo Kanisa sio
kubaki tu katika kufikiria mambo ya kiroho. Mkutano huo pia ulifanya uchambuzi
kwa jinsi gani wanaweza kukabiliana na hali halisi za kijamaa na kupendekeza mbinu
chanya na utendaji kuelekea hali halisi na mienendo ya kijamii.Na pia walitazama suala
la wakimbizi wanaowasili na kusisitiza haja ya kujenga mshikamano wa mataifa ya Ulaya
kwa ajili ya kukabiliana na hali hii kama ilivyojitokeza siku hizi katika kisiwa cha
Lampedusa, ili isijirudie tena na pia walijadili na mgogoro wa kiuchumi, na kutoa
jibu linalohimiza wenye navyo kuwagawia wasiokuwa navyo, watu masikini, kama Papa
Francisko alivyo himiza wakati akitembelea kituo cha Lampedusa, na katika homilia
zake kadhaa.