2013-10-08 07:59:16

Viongozi wa Africa wahimiza kusitisha watu kuhama nchi zao


AskofuMkuu Berhaneyesus Demerew Souraphiel wa Addis Ababa, akizungumza na Redio Vatican mwishoni mwa wiki alisema , viongozi wa Afrika wanapaswa kuona ni fedheheshwa na aibu kwao kushindwa kufanikisha amani, uhuru,demokrasia , nafasi za kazi na maisha ya kuvutia kwa watu wao. Askofu Mkuu huyo aliasa, kwa kurejea tukio la wiki iliyopita katika kisiwa cha Lampedusa , ambako vimetokea vifo vilivyotisha dunia, kwa wahamiaji karibia mia mbili, waliokuwa wamepania kuingia Ulaya toka Afrika, kuzama maji.

Aidha Askofu Mkuu wa Addis, amezitaka pia serikali za Ulaya, kuboresha sera zao za uhamiaji na taratibu wakimbizi, wanaoomba idhini za kuingia katika nchi zao, kama inavyotakiwa na sheria za Umoja wa Mataifa, ili kulinda haki za binadamu. Hata hivyo, aliongeza, serikali za Afrika lazima kuboresha hali ya uchumi na huduma kwa jamii, kiasi kwamba wananchi wasione haja ya kuhatarisha maisha yao kwenda nchi za mbali kutafuta maisha ahueni, na tamaa zisizo na kipimo katika kutafuta mali .

Aidha Askofu Mkuu Berhaneyesus amemetoa wito kwa vijana wa Afrika, kuwa na ujasiri wa kubaki katika bara lao na kufanya kazi pamoja ili kuboresha hali halisi ya Afrika kuliko kutoka nje ya Afrika, alisisitiza katika maelezo yake wakati akihojiwa na Padre Moses Hamugole wa Radio Vatican.










All the contents on this site are copyrighted ©.