Waathirika wa Lampedusa wakumbukwa Vatican kwa ukimya na maombi.
Jumapili, Papa Francisko, aliwakumbuka kafara na waathirika wote wa Lampedusa,
kwa kukaa kimya kwa muda wa dakika chache wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, aliyosali
mbele ya maelfu ya mahujaji na wageni , waliofika kusali pamoja katika uwanja wa kanisa
kuu la Mtakatifu Petro.
Zaidi ya watu mia wamethibitishwa kufa maji baada
ya boti waliokuwa wakisafiria kushika moto, kabla ya kufika katika bandari ya kisiwa
cha Lamepdusa, Alhamis iliyopita. Wengi wa wasafiri hao wenye asili ya Afrika, walikuwa
wakijaribu kuingia Ulaya bila kibali na kwa njia isiyo halali.
Baada ya ukimya
huo, Papa alihutubia umati wa watu waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la
Mtakatifu Petro. Na hotuba yake ilianza kwa kurejea, ziara yake ya Kichungaji Assis,
ambako pamoja na nia ya kwenda kusali, mahali alipoishi wajina wake Mtakatifu Francis,na
kukutana na watu wa Assis pia ilikuwa na nia ya kushiriki katika maadhimisho ya Sikukuu
ya Mtakatifu Francis, Oktoba 4. Papa alitrudia kutoa shukrani zake za dhati, kwa
makaribisho mazuri, waliyo mpatia watu wa Assis.
Na akitafakari Somo la
Injili ya siku , Papa alizungumzia nguvu ya imani , huku akitoa mwaliko kwa umati
uliokuwa ukimsikiliza, kurudia kwa mara kadhaa , ombi alilolitoa “Bwana, tuongezee
imani yetu”. Na aliwazungumzia wale ambao ni wepesi wa moyo na wanyenyekevu , au
wale wanao yapokea matatizo katika maisha yao kwa moyo wa unyenyekevu na kuyakubali
matatizo kama sehemu ya maisha yao, ambao hujiona si kitu mbele ya Mungu na jirani
, ingawa wana uwezo wa kufanya mambo makubwa, wenye kudumisha utulivu fulani, kwa
sababu ya imani yao.
Aidha Papa Francisko, alikumbusha Mwezi wa Oktoba, ni
mwezi uliotengwa rasmi kwa ajili na majitoleo ya namna ya kipekee kwa wamisionari
, hasa wale ambao wanapambana na vikwazo vigumu katika kuitangaza Injili. Alisema,
uwepo wao ni fundisho kwa Wakristu wote kwamba, kila mmoja katika maisha yake mwenyewe
ya kila siku, ni wakati wa kumshuhudia Kristo , kwa nguvu ya Mungu, nguvu ya imani.
Papa
alisema“Nguvu hii hupatikana kupitia maombi. Maombi ni pumzi ya imani. Katika uhusiano
ambapo kuna imani na upendo, aliendelea, kuna haja ya kuwa na mazungumzano. Maombi
ni mazungumzo kati ya nafsi ya mtu na Mungu”.
Aidha Baba Mtakatifu alikumbusha
pia, Oktoba ni mwezi wa Rozari ,kama ilivyo katika Kalenda ya Liturujia, ikianza
na Jumapili ya kwanza ya mwezi huu. Kumwomba Mama Yetu wa Pompei , Mbarikiwa Bikira
Maria wa Rosari Takatifu. Papa Francisko ameeita Ibada ya Rozari, kuwa ni "shule
ya sala ," na " shule ya imani! "
Na baada ya sala la Malaika wa Bwana, Papa
alizungumzia Rolando Rivi , mseminaristi mwenye miaka 14, shahidi wa imani, aliyeuwa
mwaka 1945, ambaye alitangazwa Mwenye Heri Jumamosi iliyopita, huko Modena Italy
. Papa alisema jinsi gani kijana huyu ni mfano mkubwa kwa vijana wa leo . "Yeye
alijua ambapo alikuwa na kwenda ... alijua upendo wa Yesu katika moyo wake, na alitoa
maisha yake kwa ajili upendo huo wa Yesu. Papa Francis alihitimisha tukio hili
la Sala ya Malaika Bwana kwa kumtakia kila mmoja Jumapili njema.