2013-10-04 08:57:47

Siku ya Upashanaji habari Duniani 2014


Siku ya upashanaji habari duniani ya mwaka 2014, inaadhimishwa kwa lengo la kutazama kw amakini zaidi, uhusiano kati ya mawasiliano na utamaduni wa mahusiano. Hii ni inaashiriwa na mada iliyotolewa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya siku ya upashanaji habari duniani. Mada yenyewe ni: Mawasiliano katika huduma ya mahusiano ya kweli ya tamaduni.
Kulingana na Kamati ya kipapa kwa ajili ya mawasiliano ya kijamii, binadamu hujieleza na kuendeleza mahusiano yake kwa njia ya mawasiliano. Uwezo wa kuwasiliana vyema unahitaji unyofu, uadilifu, unyenyekevu na heshima kwa wengine; pamoja na nia na jitihada ya kuweza kujifunza kutoka kwa wengine. Zaidi ya yote, mawasiliano ni maarifa yanayohitaji mazungumzo na majadiliano katika ukweli. Ni katika kufanya hivyo ambapo binadamu ataweza kutambua kumbe tofauti zilizomo kati ya watu ni utajiri mkubwa kwa jamii ya binadamu. Na katika kutambua jambo hilo, mwanadamu pia anatambua na kuelewa ukweli sio tu wa wengine, hata zaidi, ukweli juu ya nafsi yake mwenyewe.
Dunia kwa sasa hivi inapitia utamaduni mpya, linasema gazeti la kila siku la Osservatore Romano, lenye kuchpishiwa mjini Roma. Utamaduni huo mpya unaendelezwa na teknologia, na hivyo mawasiliano yamepanuliwa na yanaendelea kukua na kupanuka.
Ni mwaliko kwa jamii nzima kuendeleza mawasiliano ndani ya mtazamo mpya, kwamba licha ya mahusiano ya kibinafsi, mawasiliano hutoa pia nafasi muafaka kwa jamii nzima kuweza kuonja utamu na urembo wa kutembea pamoja kama jamii ya kizazi kipya, kwenye safari ya maisha na safari ya kiroho. Urembo wa kiimani na hata wa kukutana na Kristo, kama alivyobainisha baba mtakatifu Francisko alipokuwa akiongea na waliohudhuria mkkutano wa hivi karibuni wa Kamati ya kipapa kwa ajili ya mawasiliano ya kijamii, uliofanyika mjii Roma na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Kanisa kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Hivyo Tema ya siku ya upashanaji habari duniani mwaka 2014 inatoa changamoto na inawaalika wote wenye kujihusisha na mawasiliano ya kijamii kuzingatia ukweli, usahihi na uthabiti wa yale wanayowasilisha kwenye jamii, huku wakizingatia maadili na imani yao ya kikristo wanayoiishi ndani ya tamaduni mambo leo. Huu ni mwaliko pia wa kuzingatia lugha mwafaka kwa ajili ya kuyafikia malengo ya mahusiano na ushirikiano kwenye jamii.
Uwezo wa kuwasiliano unaonekana kwenye ubunifu katika kuafikia ushirikiano na upendo katika mwuungano kama ule wa utatu mtakatifu; ambayo ni zawadi inayowasaidia watu kukua katika mahusiano binafsi, na kuendeleza majadiliano kama jibu muafaka dhidi ya utengano unaoletwa na chuki, uhasama na migogoro ndani ya jamii na kati ya mataifa.
Ulimwengu wa utandawazi unaashiria kasi ya uwezo wa mawasiliano kufikia kona zote za dunia, za ulimwengu halisi; unaashiria pia kasi hiyo hiyo ya mawasiliano kwenye ulimwengu “ulioumbwa” na tecknologia; ulimwengu wa mitandao ya kijamii. Hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha uwepo wa mawasiliano bora hata kwenye mitandao ya kijamii na kuendeleza usikivu, majadiliano ya kina na matumaini, kama anavyopendekeza Papa, ili kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma katika kuendeleza mahusiano mema na mawasiliano ndani ya jamii.
Ujumbe unaotolewa na mada ya siku ya upashanaji habari duniani kwa mwaka 2014 inatafuta kuchunguza ukuu wa mawasiliano kwenye ulimwengu ambao unaendelea kwakaribia watu wake zaidi na zaidi kwa njia ya mitandao, ili kuhakikisha kwamba mitandao hiyo inarahisisha na kuboresha mahusiano na ukaribianaji wa watu kwenye ulimwengu unaozingatia haki na usawa zaidi kwa watu wake.
Siku ya upashanaji habari duniani ilianzishwa na Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatikani kupitia hati ya Inter Mirifica, na inaadhimishwa kila mwaka kwenye Jumapili ya Pili baada ya Maadhimisho ya Pentekoste.











All the contents on this site are copyrighted ©.