2013-10-04 09:06:29

Makumi ya wahamiaji wafamaji Mediterrania


Dunia nzima inaendelea kuomboleza vifo vya watu zaidi ya 80 kwenye bahari ya Mediterranean. Na kwenye pwani ya Lampedusa, iliyomo kusini mwa Italia, zaidi ya watu 500 wakiwemo watoto 30 wametua nanga wakiwa ni wakimbizi kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanayoyakimbia mateso na mahangaiko yatokanayo na migogoro kwenye nchi zao.
Naye Baba Mtakatifu Francisko anasema dunia ya kimataifa na mashirika ya Umoja wa Ulaya na nchi husika kwenye umoja huo, hazina budi kulipa kipaumbele cha kwanza tatizo linaloendelea kuikumba pwani ya Lampedusa kutokana na idadi ya watu wanaotia nanga kisiwani humo kila siku, wengi wao wakiwa wamesafiri miezi mingi baharini huku wakikumbwa na hatari ya kuzama au kufa njaa baharini.
Nayo serikali ya Italia imeendelea kuiomba jumuiya hiyo ya ulaya kuingilia kati na kutoa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya waathirika wanaofikia nchini humo na ambao wanahitaji ulinzi wa kimataifa. Serikali hii inauomba umoja huo kuwakubali wakimbizi kufikia nchi zao kwa njia halali ya kisheria ili kuthibiti tatizo la kuhatarisha maisha kwa kuyalipa makundi haramu ili kuwasaidia kufika ulaya.
Walinda usalama kisiwani Lampedusa wamekuwa wakiwaokoa watu wengi wanaofikia kisiwani humo kila siku. Hata hivyo, vifo vya watu 80 vimewafanya walinda usalama hao kutafakari juu ya njia iliyo bora zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo.
Naye Padre Giovanni La Manna sj, rais wa kituo cha wakimbizi cha Astalli, kinachoendeshwa na mapadre wa shirika la Yesu au Wayesuiti, nchini Italia anasema kwamba ni wajibu wa watu wote kukabiliana na changamoto hiyo. Anasema padre Giovanni kwamba ni aibu kwamba mwaka 2013, watu wengi hivyo wanaendelea kuyahatarisha maisha yao kwa kusafiri kinyume cha sheria kwenye bahari ya Mediterenian. Anasema Padre huyu ni vyema kuwapokea watu hao kihalali wakiwa hai, kuliko kuwapokea kuwapokea wakiwa maiti, huku akilaani biashara haramu ya binadamu inayoendeleza tatizo hilo.
Naye baba Mtakatifu Francisko, akitumia mtandao wa kijamii wa Twitta, ametuma ujumbe wa rambirambi kwa ajili ya wote waliopoteza maisha yao kwenye tukio hilo.











All the contents on this site are copyrighted ©.