2013-09-21 15:31:41

Papa afanya mabadiliko na kuwathibitisha wengine katika nafasi zao, katika ofisi za curia ya Roma


Baba Mtakatifu anaendelea kuteua majina mapya na kuthibitisha wengine katika kazi zao kwenye ofisi za curia ya Roma.

Jumamosi taarifa imetolewa kwamba: Baba Mtaktifu Francisko, amekubali ombi la kujiuzuru kwa mujibu wa umri, la Kardinali Manuel Monteiro de Castro, aliyekuwa Mkuu wa Ofisi Kuu ya Kitubio na katika nafasi yake, Papa amemteua Kardinali Mauro Piacenza, ambaye hadi kuteuliwa alikuwa ni Mkuu wa shirika la Mapadre Vatican.

Na Papa amemthibitisha katika kazi yake, Mkuu wa Shirika la Mafundisho ya imani Sadikifu , Mons. Gerhard Ludwig Müller , Askofu Mkuu Mstaafu wa Regensburg na Katibu wake , Luis Francisco Ladaria Ferrer, Askofu Mkuu wa jina wa Tibica, na katibu Mwambata, Mons. Joseph Augustine Di Noia , Askofu Mkuu wa Jina wa jiji la Oregon, City , ambaye mpaka sasa pia ni Makamu wa Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Kanisa la Mungu" Ecclesia Dei ". Na pia amewathibitisha wajumbe na washauri wa Baraza la Shirika hilo, pia Askofu Giuseppe Sciacca ,Askofu wa jina shirika, kuwa Katibu mwambata katika Mahakama Kuu ya Sahihi ya Kitume “Signatura Apostolica”.

Na katika Shirika la Uinjilishaji wa watu , Papa amemthibitisha Kardinali Fernando Filoni kuendelea kuwa Mkuu wa Shirika , na Katibu wake Mons. Savio Tai Fai , Askofu Mkuu wa jina wa Sila , na Katibu wake Mwambata Askofu Mkuu Protase Rugambwa , na kuwathibitisha Wajumbe na Washauri wa Baraza hilo.

Na kwa ajili ya Shirka la Makreli, Papa amemteua kuwa Mkuu wa Shirika, Mons. Beniamino Stella, Askofu Mkuu wa jina wa Midla , ambaye hadi kuteuliwa alikuwa ni Rais wa Chuo cha Kipapa cha elimu ya Kanisa , na kumthibitisha katibu wake Mons. Celso Morga Iruzubieta , AskofuMkuu wa jina wa Alba, Na pia amemteua kuwa Katibu kwa ajili ya idara inayohusika na seminari Mons. Jorge Carlos, Askofu wa Papantla ,na hivyo anapanda cheo na kuwa Askofu Mkuu .

Na katika utawala wa urithi wa Kiti cha Kitume, Papa amemteua kuwa mjumbe katika shughuli za kawaida Mons. Mauro Rivella , Padre wa Jimbo kuu la Torino.Aidha Papa amemteua Mjumbe wa Kitume nchini Ujeruman, Askofu Mkuu Nikola Eterovi_Askofu Mkuu wa jina wa Cibale, ambaye nafasi yake inachukuliwa na Mons. Lorenzo Baldisseri , Askofu Mkuu wa Jina wa Diocleziana , aliyekuwa Katibu katika usharika la Maaskofu.
.
Pia Baba Mtakatifu amemteua kuwa Nunsio nchini Sierra Leone, Mons. Miros a_aw Adamczyk , Askofu Mkuu wa Jina wa Otricoli , ambaye pia ni Nunsio wa Papa Liberia na Gambia.

Baba Mtakatifu amemteua kuwa Nunsio wa kitume na Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya elimu ya kanisa Padre Giampiero Gloder , Mshauri wa Ofisi ya ushauri maalum katika Sekretariat ya Jimbo la Papa na hivyo kupandishwa cheo na kuwa AskofuMkuu wa jina wa Telde.








All the contents on this site are copyrighted ©.