2013-09-18 10:01:24

Watu kadhaa mbaroni kuhusiana na mashambulizi ya kutumia tindikali -Zanzibar


Jumatatu Polisi kisiwani Zanzibar , ilithibitisha watu 15 kutiwa mbaroni , kwa tuhuma za kumshambulia kwa tindikali Padre Josseph Anselm Mwanagamba , Ijumaa iliyopita na shambulio jingine la mwezi uliopita kwa walimu wawili wa kujitolea kutoka Uingereza.

Kamisheni wa Polisi Zanzibar , Mussa Ali Mussa, ameeleza kuwa, baadhi ya watuhumiwa nii vijana waliokuwa wakitafuta mbinu za kuondoka kwa nia ya kwenda kujiunga na kikundi cha uhalifu cha Somalia cha al Shabab. Na wamekiri kuwa walikuwa wanakwenda kujindaa kwa jihad. Mussa amesema, Polisi bado inaendelea kuwachunguza watuhumiwa hao, na mara kesi yao itatajwa mahakamani. Na kwamba bado ni mapema mno kujua lengo la mashambulio hayo.

Jumapili , Rais wa Zanzibar , Dr Mohammed Shein, aliiagiza Idara ya polisi visiwani Zanzibar, kwa haraka, kufanya upelelezi wa kina juu ya mashambulio haya ya kutumia tindikali na wahalifu wakamatwe na kufikisha mbeleya sheria mara moja. Dr Shein alitoa agizo hilo, wakati akimtembelea Padre Anselmo Mwangamba aliyemwangiwa tindikali na mwili wake kudhurika na kulazwa katika hospitali ya hospitali ya mnazi mmoja mjni Zanzibar.

Dr Shein alisema , shambulio kama hili ni unyama wa hali ya juu kufanyika katika jamii iliyostaraabika , na hivyo serikali yake haiwezi kuwavumilia wahalifu kama hao. Na aliwataka Wakatoliki na wakristu kwa ujumla na watu waliostraabika, kuwa na uvumilivu , wakati serikali inalishughulikia suala hili.

Padre Mwanagamba kwa wakati huu amelazwa katika wodi ya Kibasiri ya Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Muhimbili, iliyoko jijini Dar es Salaam.

Na Kesi ya Ponda yaahirishwa hadi Oktoba
Na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imemnyima dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, anayekabiliwa na mashtaka ya kukaidi amri halali, kuharibu imani za dini, kushawishi na kuchochea vitendo viovu katika jamii.


Ombi la kumnyima dhamana lilitolewa na Wakili wa Serikali, Bernad Kongola, akidai kuwa DDP kwa sababu ya maslahi ya nchi na usalama wake mwenyewe.


Ombi hilo lilisababisha mvutano wa kisheria kati ya upande wa mashitaka na upande wa utetezi hali iliyomfanya Hakimu Kabate kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba mosi, ili kupitia vifungu vya sheria kuona uwezo wa kusikiliza shitaka hilo ama shitaka hilo lifunguliwe katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kuimarishwa ulinzi katika eneo la Mahakama, pia barabara zinazokatisha mahakamani hapo zilifungwa hali iliyosababisha kusimama kwa muda kwa shughuli katika ofisi za serikali zilizopo mahakamani hapo ikiwemo ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ofisi ya Hazima Ndogo na Madini.


Wafuasi wa Ponda, kabla ,katika msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja uliopo katika eneo la Kiwanja cha Ndege, walifanya mkesha wa itikafu iliyosomwa kwa ajili ya kuomba kiongozi huyo ashinde kesi inayomkabili.








All the contents on this site are copyrighted ©.