2013-09-18 08:32:38

Kanisa lisilo na kumbukumbu ni kanisa feki

Kanisa lisilo na kumbukumbu ni kanisa ishia, lisilo na uhai! Ni changamoto aliyoitoa Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu wakati wa mkutano na Mapadre wa Jimbo lake la kipapa la Roma, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohanne Laterano. Baba Mtakatifu alikuwa akiongelea juu ya pendo la kwanza la Padre, ambalo ni Yesu Kristo mwenyewe. Kwa kumsahau mpenzi wake, Yesu Kristo, Padre huingia kwenye hatari ya kutafuta pendo lisilo la kweli na la kudumu. Hivyo aliwaasa mapadre daima kurudi kwenye penzi la kwanza, Yesu Kristo.
Amesema Baba Mtakatifu kwamba ni katika kumrudia Kristo tu, Padre anaweza kupata faraja maishani mwake, kwani Kristo ndiye daima mwenzi wa maisha ya Padre, kwani safari ya kiroho hufanyika barabarani – katika kuyaishi maisa - na wala sio kwenye maabara, asema Papa, hivyo ni muhimu daima Padre kujirudi na kuirejelea barabara huku akishikana mkono na mapadre wenzake na watu wote wenye mapenzi mema.
Baba Mtakatifu aliwafurahisha mapadre wake wa Roma ambao walimshangilia kwa furaha alipowaambia kwamba yeye anajisikia kwanza kabisa kuwa Padre, halafu baadaye Askofu, na kwamba anamshukuru Mungu kwamba hajisikii kuwa wa maana zaidi kuliko Padre mwingine yule.
Jibu hilo lilitokana na swali kutoka kwa mmoja wa mapadre aliyetaka kufahamu vipi anajisikia Jorge Mario Bergolio akiwa Papa kwani kama Askofu mkuu wa Buenos Aires alizoea kujiita Padre na wala sio Askofu. Aliwaomba mapadre wake kumtahadharisha mara moja ikiwa hata mara moja watamwona yeye akijisahau na kujikweza au kujisikia mkuu kuliko wao.
Baba Mtakatifu amewahimiza mapadre kupendana kwa dhati na kuwapenda pia maaskofu wao. Maaskofu nao wawapende sana mapadre wao kwani ndio walio karibu zaidi kama wachungaji wenza.
Hili lina maana kubwa kwani mapadre huchoka sana kwenye ziara yao ya kitume. Lakini, asema Baba Mtakatifu uchovu huo usiwe kisababu cha wao kukosa kuwa karibi na mpenzi wao Yesu kristo. Amewahimiza kuitembelea tebanaklo Takatifu kila siku baada ya ziara zao za kitume, ili kumsalimu Kristu kwenye fumbo la mkate, huku akisema kwamba uchovu hauwezi kuepukika ikiwa padre anafanya kweli kazi yake ya kukutana na watu wa Mungu. Hata hivyo, ameonya Baba Mtakatifu kwamba Padre anaweza pia kupata uchovu kutokana na kutelekeza wajibu wake wa kuwa karibu na watu wa Mungu. Dawa ya uchovu wa aina hiyo, anasema Papa, sio kumeza vidonge, bali kumrudia Mwenyezi Mungu.
Anasema baba Mtakatifu kwamba kuna pia uchovu unaomkuta mtu baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kuyachunguza maisha yake huku akipata sintofahamu ya mambo mengi yatokeayo kwenye maisha. Uchovu huu unaweza kufananishwa na ule w Yohanne Mbatizaji akiwa gerezani. Ni uchovu wa kiroho. Ni uchovu alioufananisha na giza linaloingia wakati jua linatua. Mtu hujiuliza juu ya ummaana ya yale yote aliyotenda maishani mwake – sadaka mbalimbali anazofanya padre na vitu vyote alivyojinyima kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Hata Yohanne Mbatizaji alipata uchovu huo alipokuwa gerezani na akawatuma wafuasi wake kumuuliza Yesu ikiwa alikuwa masiha waliokuwa wakimngoja au iliwapasa kuendelea kungojea. Mtu anapojipata akijiuliza kama alitenda sawa au alikosea mahali fulani. Yote haya hutokea kwa watu wengi na Baba Mtakatifu amegusia watu mbalimbali wanaotajwa kwenye Biblia waliopitia aina hii ya uchovu, kama vile Eliya na Musa, Yeremia na hata Yohanne Mbatizaji.
Hivyo papa amewapa changamoto Mapadre wa jimbo lake la Roma kuwa Karibu na Kristo daima, na kuwa na mshikamano wao kwa wao na pia na wakristo wao na watu wote wa Mungu ili kuweza kuiendeleza kazi ya kichungaji uinjilishaji mpya.

Kanisa lisilo na kumbukumbu ni kanisa kaharabu, kanisa lisilo na uhai! Ni changamoto aliyoitoa Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu wakati wa mkutano na Mapadre wa jimbo lake la kipapa la Roma kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohanne, Laterano. Baba Mtakatifu alikuwa akiongelea juu ya pendo la kwanza la Padre, ambalo ni Yesu Kristo mwenyewe. Kwa kumsahau mpenzi wake, Yesu Kristo, Padre huingia kwenye hatari ya kutafuta pendo lisilo la kweli na la kudumu. Hivyo aliwaasa mapadre daima kurudi kwenye penzi la kwanza, Yesu Kristo.
Amesema Baba Mtakatifu kwamba ni katika kumrudia Kristo tu, Padre anaweza kupata faraja maishani mwake, kwani Kristo ndiye daima mwenzi wa maisha ya Padre, kwani safari ya kiroho hufanyika barabarani – katika kuyaishi maisa - na wala sio kwenye maabara, asema Papa, hivyo ni muhimu daima Padre kujirudi na kuirejelea barabara huku akishikana mkono na mapadre wenzake na watu wote wenye mapenzi mema.
Baba Mtakatifu aliwafurahisha mapadre wake wa Roma ambao walimshangilia kwa furaha alipowaambia kwamba yeye anajisikia kwanza kabisa kuwa Padre, halafu baadaye Askofu, na kwamba anamshukuru Mungu kwamba hajisikii kuwa wa maana zaidi kuliko Padre mwingine yule.
Jibu hilo lilitokana na swali kutoka kwa mmoja wa mapadre aliyetaka kufahamu vipi anajisikia Jorge Mario Bergolio akiwa Papa kwani kama Askofu mkuu wa Buenos Aires alizoea kujiita Padre na wala sio Askofu. Aliwaomba mapadre wake kumtahadharisha mara moja ikiwa hata mara moja watamwona yeye akijisahau na kujikweza au kujisikia mkuu kuliko wao.
Baba Mtakatifu amewahimiza mapadre kupendana kwa dhati na kuwapenda pia maaskofu wao. Maaskofu nao wawapende sana mapadre wao kwani ndio walio karibu zaidi kama wachungaji wenza.
Hili lina maana kubwa kwani mapadre huchoka sana kwenye ziara yao ya kitume. Lakini, asema Baba Mtakatifu uchovu huo usiwe kisababu cha wao kukosa kuwa karibi na mpenzi wao Yesu kristo. Amewahimiza kuitembelea tebanaklo Takatifu kila siku baada ya ziara zao za kitume, ili kumsalimu Kristu kwenye fumbo la mkate, huku akisema kwamba uchovu hauwezi kuepukika ikiwa padre anafanya kweli kazi yake ya kukutana na watu wa Mungu. Hata hivyo, ameonya Baba Mtakatifu kwamba Padre anaweza pia kupata uchovu kutokana na kutelekeza wajibu wake wa kuwa karibu na watu wa Mungu. Dawa ya uchovu wa aina hiyo, anasema Papa, sio kumeza vidonge, bali kumrudia Mwenyezi Mungu.
Anasema baba Mtakatifu kwamba kuna pia uchovu unaomkuta mtu baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kuyachunguza maisha yake huku akipata sintofahamu ya mambo mengi yatokeayo kwenye maisha. Uchovu huu unaweza kufananishwa na ule w Yohanne Mbatizaji akiwa gerezani. Ni uchovu wa kiroho. Ni uchovu alioufananisha na giza linaloingia wakati jua linatua. Mtu hujiuliza juu ya ummaana ya yale yote aliyotenda maishani mwake – sadaka mbalimbali anazofanya padre na vitu vyote alivyojinyima kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Hata Yohanne Mbatizaji alipata uchovu huo alipokuwa gerezani na akawatuma wafuasi wake kumuuliza Yesu ikiwa alikuwa masiha waliokuwa wakimngoja au iliwapasa kuendelea kungojea. Mtu anapojipata akijiuliza kama alitenda sawa au alikosea mahali fulani. Yote haya hutokea kwa watu wengi na Baba Mtakatifu amegusia watu mbalimbali wanaotajwa kwenye Biblia waliopitia aina hii ya uchovu, kama vile Eliya na Musa, Yeremia na hata Yohanne Mbatizaji.
Hivyo papa amewapa changamoto Mapadre wa jimbo lake la Roma kuwa Karibu na Kristo daima, na kuwa na mshikamano wao kwa wao na pia na wakristo wao na watu wote wa Mungu ili kuweza kuiendeleza kazi ya kichungaji uinjilishaji mpya.

All the contents on this site are copyrighted ©.