2013-09-17 09:05:26

ni nini kilichofichika katika mashambulio ya tindikali Zanzibar ?


Serikali ya Tanzania imehimizwa kutotegemea tu jeshi la polisi kupambana na mashambulio yanayofanywa dhidi ya watu mbalimbali Zanzibar, bali itafute mbinu nyingine mpya ya kuwanasa wahalifu hao, kwa mfano kuunda tume maalum kwa ajili hiyo. Mhariri wa gazeti la The Guardian Tanzania, ameishauri serikali kufuatia shambulio baya la kumwagiwa tindikali Padre Mkatoliki Ijumaa iliyopita, ukiwa umepita mwezi mmoja tu tangu kulipo fanyika shambulio jingine kama hilo, kwa wasichana wawili wa Uingereza kumwangiwa tindikali na wtu wasiojulikana.

Mpaka sasa hakuna mtu au kundi linalodai kuhusika na mashambulio hayo wala kutajwa lengo na nia za vitendo hivyo viovu vilivyo nje ya ubinadamu.

Mhariri wa The Guardian katika tahariri yake ya Jumapili alisema, wao mpaka sasa hawana vithibitisho kama mashambulio haya ni kwa sababu za kidini , lakini ni wazi mazingira ya mashambulio yanayonyesha ni vikundi vya wababe wasiovumilia wenigne. Na cha kusitisha zaidi, mpaka sasa hakuna waliokwisha kamatwa kuhusika na matukio licha ya polisi kuahidi donge nono la fedha, kwa atayeisadia polisi kuwanasa watu hao. Kutokamatwa kwa wahalifu kunatia wasiwasi kama kweli polisi iko makini katika kuwatia mbaroni wahalifu hao.

Katika mazingira hayo, Mhariri wa The Guardinai Jumapili alitoa ombi lake kwa serikali kuunda tume maalum wakiwemo watalaam kutoka idara mbalimbali kwa ajili ya kupata kiini cha sababu ya mashambulio hayo Zanzibar.

Rais wa Zanzibar , Dr Mohammed Shein, Jumapili aliiagiza Idara yapolisi katiak visiwa hivyo kufanya upelelezi w akina ju ya mashambulio haya ya kutumia tindikali na wahalifu wakamatwe na kufikisha mbeleya sheria mara moja. Dr Shein alitoa agizo hilo, Jumapili wakai akimtembelea Padre Anselmo Mwangamba wa Kanisa Katoliki, aliyemwangiwa tindikali na watu wasiojulikana na kwa wakati huu amelazwa ktiak hospitali ya mnazimmoja mjni Zanzibar.

Dr Shein alisema , shambulio kama hili ni unyama wa hali ya juu unaoweza kufanyika tiak jamii iliyodtaraabika , na hivyo serikali yake haiwezi kuwavumilia wahalifu kama hao , na polisi ni lazima wafanye kila jitihada kuwapata wahalifu hao. Na akizungumza na baadhi ya Wakatoliki waliofika hospitalini kumjulia hali Padre Alnselm , Dr Shein aliwataka wawe na uvumilivu , na serikali itahakikisha wahalifu wnatiwa mbaroni.

Nalo gazeti la This Day limetaarifu kwamba, baadaye Padre Anselmo, ambaye asilimia 30 ya mwili wake umeathiriwa na tindikali, hasa sehemu za usoni , alihamishiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Muhimbili Dar-es Salaam na kwamba kwa bahati macho yake hayakudhurika . Padre Anselmo amelazwa katika wodi ya wagonjwa ya Kibasila, kwa matibabu zaidi.








All the contents on this site are copyrighted ©.