2013-09-14 10:01:15

Papa asema hakuna uzushi ulio mwema bali ni uuaji


Papa amesema, uzushi na uongo ni uhalifu kwa sababu ni kumuua Mungu na jirani

Mtu mwenye tabia ya uzushi, muongo na kizabinazabina, mpenda kusema mabaya ya wengine, mtu huyo ni mnafiki ,asiye kuwa na ujasiri wa kuangalia mapungufu yake wenyewe. Ni onyo lililotolewa na Papa Francesco, katika Ibada ya Misa asubuhi, siku ya Ijumaa , ibada aliyo adhimisha katika katika kanisa ndogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.

Ujumbe wa Papa katika homilia yake , ulikemea tabia ya uongo na kuvumisha ya wengine,akisema hiyo ni dhambi na uhalifu kwa kuwa kila mara tunapo wasema vibaya wengine , ni kuwadhuru , ni kitendo cha kuua kama ilivyokuwa kwa Kaini.

Papa Framcisko alieleza akirejea Injili ya Siku : Lk 6; 37 42 ambamo Yesu anafundisha na kukataza kupigia debe makosa au mapungufu ya wengine, badala yake, tunapaswa kwanza kuchunguza kwa kina mapangufu yetu wenyewe kabla ya kutuhumu wengine( kwa nini unatazama kibazi kilichoko katika jicho la mwenzako, na hapohapo huoni boriti kuwba iliyo katika jicho lako mwenyewe).

Papa Francisko aliendelea kufafanua kwamba, Yesu katika hili anamtaka kila mtu achunguze dhamiri yake mwenyewe kila wakati. Baada ya kuzungumzia unyenyekevu , Yesu sasa anatazama tabia zilizo kinyume na upendo wa Mungu, chuki kwa wengine na kuhukumu wengine . Yesu anaiitaja tabia hiyo kwamba ni unafiki .
Wale ambao daima ni kuhukumu wengine , kuzungumzia mapungufu na mabaya ya wengine, ni wanafiki, kwa sababu wao hawana nguvu ,wala ujasiri wa kuangalia makosa yao wenyewe. Yesu hazungummzi mengi juu ya hili, ila anatoa msisitizo kwamba, mbegu ya chuki dhidi ya ndugu yako ni uuaji ... Hata mtume Yohana , katika barua yake ya kwanza , anasema, wazi: anayemchukia ndugu yake anatembea gizani , na yeye mwenye kuhukumu ndugu yake, anatembea gizani (1Yn: 9-11).

Kila mara tunapo wahukumu wengine hata ndani ya mioyo yetu, tunatenda dhambi Vivyo hivyo tunapo hukumu Wakristu wengine katika utendaji wao, tunakuwa wauaji.

Papa alieleza na kusema , si maneno yake mwenyewe lakini ni Maneno ya Bwana mwenyewe kwamba , ni kumuua Mkristu, na hatuwezi kulibadili hili, bali tunapaswa kutambua kwamba, kila tunapomzunguzia mwingine vibaya ni kuua. Ni sawa na kumwinga Kaini, muuaji wa kwanza katika historia . "


Papa aliongeza, kwa wakati huu ambamo tunazungumzia vita na kuomba sana amani kwa bidii, tunapaswa na ni muhimu kwanza kujichunguza madhaifu yetu weneywe , kuungama na kujitakatifusha., na kujiepusha na porojo na uzushi na uchochezi, kwa kuwa kupenda hayo, daima, ni kutembea katika njia inayoelekea kwenye uhalifu.Hakuna uzushi usiokuwa na hatia. Mazunguzo na ma, Mtume Yakobo anasema, na iwe sifa na utukufu kwa Mungu . Lakini pale ulimi wetu unapokuwa wa kusema mabaya wengine, ndugu zetu, iwe kwa kaka au dada zetu , ni kumuua Mungu aliyemo katika sura ya binadamu, kwa ndugu zetu. Kamwe hakuna mtu anayeweza kusifiwa kwa tabia ya uzushi .

Papa ameeleza na kusisirtiza umuhimu wa kuwa na roho wa kupenda kusali na kuomba msamaha wa Bwana kwa Makosa yetu. Kufanya toba na kurejesha mahusiano na Bwana. Na kisha, kama ni lazima, kutafuta namna za kujipatanisha na tunaowakosea au kutukosea , kama mtume Paulo alivyokiri udhaifu wake akisema , kabla, mimi nilikuwa kafiri na mtesaji na mdhulumaji mkubwa. Lakini Mungu alinionea huruma, na kunikokoa. Na ndivyo nasi tulivyo, tulikuwa wadhulumaji na watesaji wakubwa, lakini sasa Bwana ametuonea huruma na kutuokoa.

Basi na tusali kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajii ya kanisa lake lote , atujalie neema ya uongofu kutoka dhambi ya uzabinazabina, uhalifu na ghasia dhidi ya neema ya uongofu , neema ya upendo dhidi ya uzushi, neema ya unyenyekevu, upole , wema, na upendo makubwa kwa jirani .








All the contents on this site are copyrighted ©.