Papa ahimiza imani katika uwezo wa kuokoa wa Msalaba
Ijumaa , Baba Mtakatifu Francisko aliwapokea na kuwahutubia wajumbe kutoka Jumuiya
ya ulinzi wa Kaburi Takatifu la Jerusalem , ambao wako Roma kwa ajili ya Mkutano wao
wa Mashauriano. Jumuiiya hii ya tangu karne za kale, ina kanuni ya kuwa na mkutano
wake mkuu kila baada ya miaka mitano,kwa lengo la kutafakari kwa kina nia za jumuiya
na hali ya jumuiya Katoliki katika Nchi Takatifu , na kutathimini zake juhudi mbalimbali
katika utendaji wa Jumuiya , hasa masuala yanayohusiana na utawala, mamlaka na mipango
kwa siku za mbele . Baba Mtakatifu akizungumza na washiriki wa mkutano huu, mjini
Vatican, alilenga zaidi nguzo tatu za maisha ya Mkristu, kuwa ni, kusafiri , kujenga
na kukiri imani, ambayo yamekuwa msingi wa mafundisho ya utawala wake tangu alipochaguliwa
kuwa Papa na Makardinali wenzake miezi sita iliyopita. Papa aliwaambia safari
yenu , iko katika historia ya dunia ambayo mipaka yake daima hupanuka na vikwazo vingi
kuanguka na mapito yenu daima yakifungamana zaidi na zaidi katika upendo wa mmoja
kwa mwingine. Na hivyo aliwahimiza Wanajumuiya wa Ulinzi katika Kaburi Takatifu, kuziishi
karama na mapokea ya utamaduni wao kwa uaminifu, unyenyekevu na upendo katika huduma
ya kujenga yaliyo bora zaidi kwa siku za usoni , na kwa ajili ya mshikamano na Wakristu
wa Nchi Takatifu katika mapambano yanayowakabili. Papa aliendelea kuwaasa kwamba,
mwendo wao katika kumfuasa Kristu ni lazima uchipuke ndani na kukua ndani ya mioyo
yao kwa kuikiri imani kwa uaminifu zaidi , na kukua katika juhdui zote zinazolenga
kuilisha roho ya maisha ya imani, aliyechipushwa na majiundo ya muda mrefu ya roho
wa Kikristu katika umoja na mshikamano wa kweli wa maisha na Kikrstu. Aidha kuamini
kaiak uwezo wa Msalaba na ufufuko wa Bwana , Papa alisema, ni kujenga tumaini na amani
katiak maisha. Na namna ya pekeee Nchi ya Yesu inahitaji uwepo wao zaidi na zaidi.
Papa aliwataka wasijitenge mbali na uwajibikaji , bali daima imani na iwe kichocheo
na msukumo wa kuwajenga imara zaidi katika utendaji wa kazi katika tumaini la kuwa
na jamii iliyo bora zaidi.