2013-09-13 16:12:21

Ratiba ya Ibada za Kiliturujia za Papa kwa mwezi Septemba hadi Novemba 2013.









Ofisi ya Ibada za liturijia za Kipapa,imechapisha ratiba ya Ibada zitakazoongozwa na Papa tangu Septemba hadi Novemba 2013 kama ifuatavyo:

SEPTEMBA:

Jumapili 22: Ziara ya Kichungaji Cagliari na katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Bonaria.

Jumapili 29: Jumapili ya 26 katika kipindi cha kawaida cha mwaka, majira ya saa nne na nusu , Papa ataongozaa Ibada ya misa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Makateksta.

Jumatatu 30: saa nne na nusu ,za asubuhi, katika Ukumbi wa mikutano ya maalum ya Makardinali au consistory, Vatican, Papa ataongoza Mkutano wa kawaida wa Consistory kwa ajili ya kutaja majina ya watakaotangazwa hivi karibuni katika orodha ya watakatifu.



OCTOBER

Ijumaa tarehe 4: Papa atafanya ziara ya kichungaji Assisi.

Jumamosi , Saa sita mchana ataongoza Ibada ya sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.

Jumapili 13: Jumapili ya 28 katika kipindi cha kawaida cha mwaka , saa nne na nusu asubuhi, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Pètro katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Maria.

Jumapili 27: Jumapili ya 30 katika kipindi cha kawaida, Majira ya saa nne na nusu, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Familia..



NOVEMBA

Ijumaa 1: Siku Kuu ya Watakatifu wote, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika eneo la Makaburi la Verano.

Jumamosi 2: Siku ya Marehemu wote, saa 12 Jioni , Papa ataongoza Ibada katika eneo la Makaburi la Vatican kwa nia ya kuombea Marehemu Mapapa wote.

Jumatatu 4: saa 5.30 asubuhi, katika Altare ya Kipapa ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , Papa ataongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Makardinali, Maaskofu Wakuu na Maaskofu waliofariki katika pindi cha mwaka mzima..

Jumapili 24: katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa ataongoza Ibada kwa ajili ya Kuufunga mwaka wa Imani.










All the contents on this site are copyrighted ©.