2013-09-12 15:45:36

Timu za Afrika zitakazochuana kwa ajili ya kombe la Dunia.


Cameroon iliigonga Libya goli moja kwa sufuri kwenye mchuano wa kung’ang’ania nafasi ya kumi na ya mwisho ya nchi zitakazochuana kwenye kombe la Dunia la Afrika mwezi ujao. Mchuano huo uliofanyika siku ya Jumapili (08/09/2013) umeipa Cameroon fursa ya kuwania moja ya nafasi tano za nchi zitakazoliwakilisha bara la Afrika kwenye Kombe la Dunia litakaolofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Nchi kumi zitakazochakachuana kung’ang’ania nafasi hizo tano ni Ivory Coast, Egypt, Algeria, Ghana, Nigeria, Senegal, Burkina Fasso, Ethiopia na Visiwa vya Cape Verde.
Timu chipukizi ya Cape Verde iliwashtua wengi hasa pale ilipoonyesha uhodari wake kwa kuishinda timu zoefu ya Tunisia kwenye uwanja wa nyumbani, hivyo kuizima ndoto ya Tunisia kuwakilisha Afrika nchini Brazil. Ethiopia nayo haijawahi kucheza kwenye Kombe la Dunia licha ya kuwa mmoja wa waanzilishi wa mpira wa miguu Afrika. Wao pia walionyesha uhodari wao pale walipoipiga Jamhuri ya Afrika ya Kati hivyo kuhitimu kwenye kundi A na kuwasukumiza nje wenyeji wa Kombe la Dunia la mwaka 2010, Afrika Kusini.
Sasa macho yote ya bara Afrika yako kwenye timu hizo kumi na kila mmoja wazo ana matumaini ya kuwa kati ya timu tano zitakazoichezea Afrika kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta bingwa wa dunia hapo mwaka kesho.








All the contents on this site are copyrighted ©.